Aibu~Hivi Ndivyo Safari ya David Moyes Ilivyokuwa Baada ya Kufukuzwa Man U


Baada ya Moyes kumalizana na Man United na
kuvunja mkataba, hakuna ubishi ilikuwa ni
lazima aondoke na kwenda kupumzika nje ya
England.
Moyes alichagua Marekani, aliona ingekuwa
sehemu nzuri ambayo angeweza kujipumzisha
kabla ya kuanza upya maisha ya mapambano.
Kwa kuwa aliamua kwenda katika Mji wa
Florida akiwa na mkewe na baada ya kulijua
hilo, bilionea Glazer alimpa Moyes ofa nyingine
ya kufikia katika nyumba yake ya kifahari iliyo
mjini humo.
Pia atapata huduma ya usafiri na usimamizi wa
kutembezwa sehemu mbalimbali za jiji hilo na
wasaidizi wa Glazer.
Utaona hivi, kocha akivunja mkataba au klabu
kufanya hivyo. Basi uadui unatangulia na
ikiwezekana viongozi wa klabu hawataki hata
kuzungumza na kocha kwa kuwa anaonekana
kama ni adui.
Glazer ndiye anayepitisha uamuzi wa mwisho,
lakini anaonyesha kiasi gani walivyoachana
kistaarabu na Moyes na hakuna tatizo lolote
lililotokea.
Hivyo mambo yako kitaalamu zaidi ndiyo maana
wakati mashabiki wanaendelea kupiga kelele.
Moyes anakula ‘bata’ Marekani.
Fin.
Moyes amelipwa fedha hizo ambazo
zinajumuisha mshahara wake wa mwezi, fedha
ya kuvunja mkataba pamoja na malipo ya
usumbufu kutokana na uvunjani huo wa
mkataba.
Lakini wakati wa uvunjani mkataba wake, kuna
mambo kadhaa ya kiufundi yalifanyika ambayo
yanaashiria namna gani walioendelea katika
michezo, mikataba yao inavyokuwa na
utaalamu.
Katika mkataba wa Moyes, ilikuwa hivi. Kama
angeifikisha timu katika nne bora na kuweza
kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi
wakimfukuza ilikuwa ni lazima alipwe kitita cha
pauni milioni 9 (zaidi ya Sh bilioni 22.5).
Pamoja na maji kuwafika shingoni, uongozi wa
Man United uliendelea kufanya subira katika
jambo moja. Kuwa iwapo watafungwa mechi
itakayothibitisha kuwa hawatakuwa katika nne,
maana yake wamekosa kushiriki Ligi ya
Mabingwa Ulaya, hapo watatoa pauni milioni 7
badala ya milioni 9.
Mkutano wa mwisho waliofanya wamiliki wa
Man United, Joe Glazer na wenzake ilikuwa ni
kujaribu kuokoa pauni hizo milioni 2 wakati
Moyes anaondoka.
Mechi dhidi ya Everton ndiyo ilikuwa na majibu,
kama Man United wangepoteza maana yake
uhakika wasingefika nne bora na malengo ya
uongozi kuokoa pauni milioni 2 ungekuwa
umetimia.
Baada ya Man United kufungwa mabao 2-0,
viongozi wa Man United waliandaa mkutano
mara moja kumtaarifu kocha huyo kuhusiana na
suala hilo na taarifa zikaanza kuvuja.
Huenda wengi walishangazwa na namna ungozi
wa Man United ulivyochelewa kumuondoa.
Lakini mambo mawili yalikuwa ya msingi zaidi
kwao kuliko matakwa ya mashabiki.
Kwanza kuangalia kama kungekuwa na
mabadiliko ili Moyes aendelee, lakini
kuhakikisha kama imeshindikana, basi na pauni
milioni 2 ambazo si haba, ziokolewe.
Hilo ni moja la kujifunza kwa klabu za hapa
nyumbani namna ambavyo mikataba
inaandaliwa kitaalamu na inakuwa imelenga
mambo kadhaa na hata ukivunjika. Zaidi
unalenda kwenye kufanikiwa na kufeli na si
ilimradi mkataba tu wa kazi, hata wa kocha
unaringana na wafanyakazi wote!
Kitu cha pili cha kujifunza ni

INSTAGRAM YAMLAZIMISHA RIHHANA KUTOA PIC ZAKE ZA UCHI INSTAGRAM

Tarehe 30 April, 2014 - Mtandao wa
Instagram wa mlazimisha Rihanna kuondoa
picha zake alizo post akiwa uchi.
Rihanna alilazimishwa kuondoa picha zake
chafu alizo post akiwa uchi kwenye mtandao
wa Instagram baada ya mtandao huo wa
kijamii kutishia kuifunga akaunti yake endapo
hata fanya hivyo.
Wiki hii Rihanna amekuwa akiweka picha
zake mbali mbali alizopiga katika photo shoot
mbalimbali huku akiwa uchi sehemu karibu
zote za mwili wake na kuziweka kwenye
mitandao ya kijamaii kama Instagram na
twitter.
Picha kama hizo zina kiuka sera na taratibu
za tovuti ya Instagram kitu kama hiki pia
kiliwahi mkuta "Madonna" na akajifunza
haraka sana baada ya kukiuka taratibu za
mtandao huu hapo mwaka jana.
Lakini kwa upande wa Rihanna yeye hakujali
sana bali alichokifanya ni kuifuta na kwenda
kuipost tena Kenye mtandao wa twitter.
Picha zenyewe zilizo zuiliwa na Instagram ni
hiz hapa..

Wezi kukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'


Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja
wa matajiri wakubwa duniani
Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa
Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za
kiisilamu.
Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni
jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo
itaanza kutumika kuanzia wiki hii.
Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni
pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga
mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya
kushiriki Zinaa.
Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika
kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi
wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za
kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na
Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na
utumiaji wa pombe.
Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha
Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah
na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje
mafuta na gesi yake.
Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika
nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza
ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo
akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha
wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria
hiyo.
Sheria yenyewe itaanza kutumika katika kipindi
cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya
kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa
faini.
Katika awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza
kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia
ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa
mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja.
Sultani anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa
matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya
watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia
mitandao ya kijamii.
Mfumo wa sheria katika mahakama nchini humo
ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha
mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo
inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki
za binadamu.

Source: BBC

UDAKU NI SHEEEDA

TAARIFA YA MWANAUME TAPELI HAPA BONGO LIVE FROM RACHEL TEMU ONA HAPA!!


Rachel A. Temu
9 hrs ·
Hello wanazuoni wa Face Book kuna kijana mjini
hapa Dar Es Salaam anajiita Moses, jina la
mwisho sijalipata vizuri mwenye namba ya simu
255 787 762168. Anadai anafanya wizara ya
nishati na madini viwanja vyake vya mtoko ni
huko Oysterbay na Masaki.
Anadai anaishi Upanga.
Huyu Kijana ni TAPELI aliyekubuhu kushinda
hata gume gume aliyewashinda mitume.
Anatarget wasichana warembo ambao ni working
class and highly cooperate.
Anaangalia kama msichana ana gari nzuri na
mwenye mvuto na akikukaribia anajidai anataka
kufanya biashara ya spare part. Huyu kaka ni
mwizi yupo na mwenzie anayesema anafanya
kazi vizazi na vifo kumbe si kweli.
Kaka William William J. Malecela na Jestina
Meru naomba watu kama hawa watangazwe
kwani wanatumia madawa kuwaibia
wanawake.This is just a warning.
Huyu Mburullaaaaaz fanfanyoko wahedi
atangazwe nanajulikane tabia zake.
This is to all beautiful girls in Tanzania.

MCHINA AJINYONGA BAADA YA KUBORONGA UJENZI WA DARAJA MOROGORO

Raia mmoja wa China ambaye ni mhandisi
katika Kampuni ya Ujenzi ya China Railway
Bureu 15 Group inayojenga Daraja la Mto
Kilombero, Qin Bao Feng amekufa kwa
kujinyonga kwa kile kinachodaiwa ni baada ya
kuboronga katika kazi.
Ilielezwa kuwa Feng aliamua kujinyonga baada
ya nguzo za daraja alilokuwa akilisimamia
katika ujenzi huo, kusombwa na maji, jambo
ambalo aliona kuwa limemvurugia kazi yake.
Baadhi ya watu waliokuwa jirani na kambi hiyo,
walisema baada ya kuharibika kwa kazi hiyo,
wahandisi wenzake kutoka China, walianza
kumtenga hali iliyomfanya ajione kuwa mpweke
na hatimaye kuchukua uamuzi huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro,
Leonard Paulo alisema tukio hilo lilitokea
Jumamosi iliyopita ndani ya kambi ya kampuni
hiyo.
Alisema mwili wa marehumu ulikutwa
ukining’inia kwenye dari ndani ya chumba
alichokuwa analala na kwamba polisi
wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio
hilo.
Kamanda Paulo alisema baada ya kuchunguza
mwili wa marehemu walikuta karatasi iliyokuwa
imeandikwa ujumbe kwa lugha ya Kichina.
Alisema kwa kuwa hakuna mkalimani aliyekuwa
jirani na eneo la tukio, polisi wanaendelea
kumtafuta mtu wa kuutafsiri.
Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo
umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis
iliyopo Kilakala, Morogoro.
Chanzo;Mwananchi

BATULI ADAIWA KUITIKISA NDOA YA MTUNIS


HABARI za motomoto kutoka vyanzo vya
uhakika , zinasema kuwa staa wa kike
anayekuja juu kwa sasa katika tasnia ya
filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘ Batuli ’
ameitikisa ndoa ya mwigizaji mwenzake , Nice
Mohammed ‘ Mtunis ’ kwa madai ya kutoka
naye kimapenzi .
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo,
Yobnesh Yusuph ‘ Batuli’.
Chanzo chetu , kwa sharti la kutochorwa jina
lake gazetini kilifunguka kuwa ishu ya wawili
hao kuwa wapenzi siyo siri, kwani mara
kadhaa wamekuwa wakijiachia sehemu
mbalimbali , huku mke wa Mtunis
akinyetishiwa, jambo lililosababisha
migongano ndani ya ndoa hiyo .
“Mmechelewa kweli kujua! Leo ndiyo
mnauliza kuhusu Mtunis na Batuli? Hao ni
wapenzi na penzi lao limenoga kwelikweli
sasa hivi . Imefikia hatua Mtunis na mkewe
hawana maelewano mazuri . Nyumba ni kama
inayumbishwa na Batuli lakini Mtunis hataki
kumwacha Batuli, ” kilipasha chanzo hicho.
Mkongwe wa filamu za Kibongo , Nice
Mohammed ‘Mtunis ’.
MTUNIS KIKAANGONI
Kama ada , Risasi Mchanganyiko lina desturi
ya kupata mzani wa habari kabla ya
kuirusha, ndivyo ilivyofanyika kwa Mtunis
ambaye aliposomewa mashitaka yake
alipovutiwa waya , alikanusha vikali akidai
ndoa yake ina amani na hana uhusiano na
Batuli.
“Kwanza nani amekuambia kuwa mimi
natoka na Batuli? Yule ana mtu wake na
mimi nina ndoa yangu. Sikia kaka , katika
kipindi ambacho ndoa yangu ina amani ni
hiki , sitaki kabisa haya mambo . Mtakuja
kusababisha Batuli agombane na mumewe
kisa mimi ,” alisema Mtunis kwa sauti ya juu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA BATULI
Batuli alipopatikana kwa njia ya simu,
alikuwa msikivu muda wote alipoelezwa
kuhusu madai hayo , mwishoni akajibu kwa
mtindo wa kuuliza : “Kwanza nikuulize, Mtunis
ni Muislam au Mkristo?”
Mwandishi wetu alipomjibu kuwa ni Muislam,
akaendelea: “Sasa kipi cha ajabu hapo ? Kwa
imani yake ya Kiislam , ana ruhusa ya kuoa
wake hadi wanne . Halafu kuna wakati
nilishaishi naye miaka si chini ya minne, kwa
hiyo sioni ajabu hapo . Hata kama ikitokea
tena hakuna tatizo.
KUITIKISA NDOA YA MTUNIS
“Achana na watu bwana, acha tu watu
waongee . Lakini ninachosema hakuna cha
ajabu hapo. Maisha yanaruhusu, yaani
kisheria hata Mungu anaruhusu - siyo ajabu.
Siwezi kuzungumza zaidi maana nimesafiri
nipo kwenye harusi , dada yangu anaolewa .”

ALIYEPIGWA NA CHID BENZ MAHUTUTI


MREMBO Mwanaisha Kiboye, mkazi wa Ilala,
Dar anayedaiwa kupigwa na mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Bongo, Rashid Makwilo ‘ Chid
Benz’ , hali imekuwa mbaya kwani yu
mahututi.
Mwanaisha Kiboye , akiwa hoi hospitali
baada ya kipigo kutoka kwa msanii Chid
Benz .
Juzi Jumatatu , wakati staa huyo
akipandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Wilaya ya Ilala, Dar kwa kesi hiyo ,
Mwanaisha alikuwa akipumua kwa tabu
kwenye chumba maalum katika Hospitali
iitwayo Aviation iliyopo maeneo hayo ya Ilala .
MAMA MDOGO ANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mama mdogo wa Mwanaisha
aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, hali
ya mgonjwa imekuwa tete kwani kwa siku
moja amekuwa akizimia zaidi ya mara tano.
Mtuhumiwa Chid Benz.
AZIMIA MARA TANO
“Mwanangu hali yake ni mbaya anazimia
zaidi ya mara tano kwa siku halafu watu
wananiambia nitoe kesi mahakamani si
nitaonekana chizi jamani ?” alisema mama
huyo huku akilengwalengwa na machozi.
Alisema hali ya mgonjwa imekuwa ikibadilika
hasa suala la presha kupanda na kushuka
huku mapigo ya moyo yakiwa chini hivyo
kuwatia hofu ndugu , jamaa na marafiki.
KIPIMO CHA KICHWA
Aliongeza kuwa siku hiyo ( Jumatatu)
madaktari na wauguzi walikuwa katika
harakati za kumpeleka kwenye kipimo
kiitwacho CT Scanning kuangalia madhara
yaliyompata kichwani na kusababisha hali
kuzidi kuwa mbaya .
Mwanaisha Kiboye akiendelea na matibabu
katika Hospitali ya Aviation, IIala.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuingia wodini
ambapo katika kipindi cha saa kadhaa
Mwanaisha hakugeuka wala kuamka kutoka
usingizini.
TURUDI KWENYE KESI
Juzi ( Jumatatu ) Chid alitakiwa kupandishwa
kizimbani Mahakama ya Mwanzo, Wilaya ya
Ilala, Dar kwa ajili ya kesi hiyo lakini
hakutokea kortini badala yake alimtuma
mdhamini wake amuombee udhuru kuwa
alikuwa akiumwa.
CHEMBA KIDOGO
Karani wa mahakama hiyo , Nusura Seleman
alipoita kesi hiyo , mdhamini huyo na ndugu
wa Chid Benz na ndugu wa Mwanaisha,
walijongea kwenye ‘ chemba kidogo’ mbele ya
Hakimu Leonia Muta .
HAIWEZEKANI
Katika kesi hiyo ambayo mwanahabari wetu
aliifuatilia hatua kwa hatua, hakimu Muta
aliwaita wenye kesi hiyo lakini wote
hawakuwepo ndipo hakimu huyo akasema
hawezi kuendelea na kesi hiyo bila wenye kesi
wote kuwepo . Shauri hilo liliahirishwa hadi
Mei 5, mwaka huu.
MAMA CHID ATOLEWA NDUKI
Akizungumza nje ya mahakama hiyo , kaka
wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina la
Swedy alisema :
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya namna ile
halafu wanatuambia tukayamalize nyumbani ,
hilo si jambo la kushangaza jamani ?
Mama yake Chid Benz alikuja nyumbani
kutaka kumuona mgonjwa tukamtoa nduki.
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya hivyo
asijekudhurika na jambo lolote akiwa
nyumbani kwetu ikaonekana tumemfanyia
kusudi .
CHID NAYE ATOLEWA BARU
“Hata Chid Benz mwenyewe naye juzi
( Jumamosi iliyopita ) alikuja na kutupigia
magoti naye tukamtoa baru, asitulee zake
kwanza hii siyo mara ya kwanza kumpiga
dada yangu kuna kipindi alimpiga kesi ilikuwa
Kituo cha Polisi cha Kilwa Road. ”
BADO HALI TETE
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni
Jumatatu jioni , bado hali ya Mwanaisha bado
ilikuwa ni tete .
Chid Benz alidaiwa kumpiga Mwanaisha Siku
ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu maeneo ya
Ilala, Dar .

MTITU AFIWA NA BABA YAKE


STAA wa filamu za kibongo William Mtitu
amepata pigo baada ya kufiwa na baba yake
mzazi , Mzee John Mtitu aliyekuwa amelazwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na
kusumbuliwa na uvimbe kichwani
Akizungumza kwa masikitiko nyumbani
kwake Mabibo jijini Dar es Salaam , Mtitu
alisema amesikitishwa na kifo cha baba yake
lakini hana jinsi kwani Mungu amempenda
zaidi na hiyo ni njia ya kila mmoja .
Staa wa filamu za kibongo, William Mtitu.
“Ninachoweza kusema ni kwamba baba
ameniachia pengo kubwa , hakuna anayeweza
kuliziba, alikuwa ni mtu wangu wa karibu na
kifo chake sikukitarajia mapema hivi ,
nimejaribu kila njia lakini safari yake ilikuwa
imeshafika, namshukuru Mungu kwa kila
jambo ,” alisema Mtitu .

WEMA SEPETU AANDIKIWA BARUA NZITO!

KWAKO,
Wema Sepetu , staa wa ukweli unayeng’ ara
kimataifa . Sina wasiwasi nikisema hivyo
maana namaanisha .
Leo nimekukumbuka kwa barua; nimefanya
hivyo mara kadhaa kila ninapokuwa na
jambo la kukushauri .
Kwanza nakupongeza kwa kutwaa taji la
msichana mwenye mvuto wa kimahaba
iliyotolewa na Gazeti la Ijumaa ‘ Ijumaa
Sexiest Girl’ wikiendi iliyopita pale Dar Live,
Mbagala – Zakhem , Dar .
Ushindi wako ni baada ya kuwaacha mastaa
wenzako wengi pembeni hadi kufikia fainali
iliyokukutanisha na Jacqueline Wolper ,
Elizabeth Michael , Jokate Mwegelo na Nelly
Kamwelu.
Vigezo vilizingatiwa lakini kubwa ilikuwa ni
kumsaka msichana mwenye mvuto kuliko
wenzake . Wema , ukijaribu kuangalia safari
yako ya mashindano ya urembo, mara zote
umekuwa ukifanya vizuri. Hujawahi
kuwaangusha mashabiki wako .
Kwanza ulivaa viatu vya Miss Dar Indian
Ocean na baadaye ukawakilisha Kanda ya
Kinondoni kabla ya kupanda Miss Tanzania
mwaka 2006 ambapo uliwabwaga wote na
kuibuka kidedea . Huo ni uwezo wa juu sana.
Nakumbuka katika kipindi kilichokuwa na
ushindani mkubwa ni pamoja na hicho.
Fainali yenu ilikuwa na wasichana wenye
mvuto na sifa hasa, lakini uliweza kupenya na
kufanikiwa kuibuka kidedea . Tangu hapo
umeendelea kuutunza vyema mvuto wako na
hujaonekana kuchuja .
Tangu mwaka 2006 ukiwa na umri wa miaka
18 ( kama ulivyosema ) , leo hii miaka nane
baadaye una miaka 26 na bado unaonekana
katika mwonekano mzuri . Hilo ni jambo zuri
na la kujivunia kwa hakika .
Kwa kuwa shindano lenyewe la Ijumaa
Sexiest Girl lilihusisha wasomaji , bila shaka
walikuchagua kwa sababu wanakukubali
katika mambo mbalimbali ya kijamii
ukiachana na mvuto ambao kilikuwa kigezo
kikuu .
Jambo kubwa kwako ni kuhakikisha
unaendelea kutunza mwonekano wako ,
unashiriki katika mambo mbalimbali ya
kijamii na kufanya vizuri katika kazi yako ya
sanaa ya uigizaji unayoifanya kwa sasa .
Lazima utambue kuwa una jina kubwa na
unakubalika; kazi yako ni kuifanya jamii izidi
kukuamini; wasione walifanya makosa
kukuchagua kwa kura nyingi ili uwe mshindi .
Nakusihi Wema , wewe ni staa , jiweke mbali
na mazingira yanayosababisha skendo . Ishi
kama kijana anayetambua thamani yake .
Wewe ni kioo cha jamii , jitahidi jamii ijiangalie
kupitia kwako.
Ijifunze mambo mengi kupitia wewe . Zile
sarakasi zako , achana nazo ili uendelee
kutunza heshima ya ustaa wako . Habari zako
magazetini acha zitawale , lakini kwa mazuri
tu ! Skendo zikae mbali na wewe .
Ukiamua, inawezekana!
Yuleyule ,
Mkweli daima,
Joseph Shaluwa

MUME, MKE WATEKWA !


KIJANA aliyetambulika kwa jina la Dickson
Mathias ( 35) , na msichana aliyejulikana kwa
jina la Mariam Kimaya wanadaiwa kutekwa
kwa nyakati tofauti baada ya kufunga ndoa
ya siri katika Kanisa la KKT , Tegeta jijini Dar ,
Mei Mosi, 2012 , Risasi Mchanganyiko
linakupa zaidi .
Mariam Kimaya anayedaiwa kutekwa.
Akizungumza na gazeti hili kwa majonzi
makubwa, dada wa Dickson, Aneth Mbaga
alisema tukio hilo lilitokea baada ya Dickson
kufunga ndoa hiyo na Mariam bila idhini ya
wazazi wake kwenye kanisa hilo.
“Baada ya habari za kufunga ndoa ya siri
kanisani kuwafikia baadhi ya ndugu wa
Mariam, Dickson alianza kupokea simu za
vitisho wakimuuliza ni kwa nini alifunga ndoa
ya siri na binti yao wao wakiwa hawajui ?
“Agosti 10, mwaka jana, nikapata taarifa
kwamba Dickson alitekwa maeneo ya Mbezi
ya Jogoo ( Dar ) na watu wasiojulikana .
Dickson Mathias anayedaiwa kutekwa
pamoja na mkewe.
Walimweleza sababu za kumteka ambazo
mimi sizijui, ” alisema Aneth.
Aneth alizidi kuongeza kuwa miezi minne
mbele , alipata taarifa kuwa , mkewe Mariam
naye alitekwa na watu wasiofahamika, hadi
sasa hajulikani alipo kama vile mumewe.
“Yeyote mwenye taarifa sahihi naomba
aripoti kituo chochote cha polisi kilicho jirani
yake maana ndugu tuna wasiwasi mkubwa,
hata kwa ndugu wa mwanamke nako hakuna
anayejua waliko wawili hao , ” alisema dada
huyo huku akimwaga machozi .
Taarifa za kutekwa kwa Dickson ziliripotiwa
katika Kituo cha Polisi Tabata na kuandikiwa
jalada: TBT /RB/1988 /2013 na polisi bado
wanawasaka wanandoa hao .

PRODYUZA MANECKY NA MADAI YA KUZAA NA RIYAMA


NYUMA ya mafanikio ya wasanii wa muziki
kuna wengi wanachangia lakini mara nyingi
ni kama hawajulikani .
Prodyuza mkali Bongo kutoka AM Records,
Emmanuel Saimon Sewando ‘ Manecky’.
Hata wakijulikana ,sifa huenda moja kwa moja
kwa msanii tu .Maprodyuza wana mchango
mkubwa sana, maana wakitengeneza ngoma
mbaya, mwisho wake ni kwamba msanii
hawezi kutoka . Leo hapa
kwenye Exclusive Interview tunaye Prodyuza
mkali Bongo kutoka AM Records, Emmanuel
Saimon Sewando ‘ Manecky ’ .
Je , unajua kuwa nyimbo kibao za wasanii
kama Diamond , Suma Lee , Ali Kiba , Keisha na
wengineo zina mkono wake?
Manecky amefafanua mengi juu ya kazi zake
za muziki , maisha binafsi na skendo kadhaa
zinazotajwa dhidi yake.
Msanii wa filamu Riyama Ally
INADAIWA DIAMOND HATAKI KUFANYA
KAZI TENA NA WEWE KWA SABABU
ULIACHIA WIMBO WAKE WA NATAKA
KULEWA BILA RIDHAA YAKE , IMEKAAJE ?
Ujue wasanii wana mchezo ukimaliza kazi
yake, anaomba demo na kuiweka kwenye
simu yake , sasa wana katabia ka kuachia
chinichini ( kwa kuwarushia rafiki zao kwa
simu) ili kusikiliza wadau wanavyopokea .
Ikipokelewa vizuri, anaitoa au akiona ina
upungufu fulani anaifanyia mabadiliko haraka ,
ndicho kilichotokea kwa Diamond .
Mimi nisingeweza kuachia singo yake bila
idhini yake .
Kwanza ili iweje ? Halafu singo yenyewe
iliyoachiwa ilikuwa haina hata lebo yangu ,
sasa ingekuwa na faida gani na mimi ?
Sijambo la kweli .
INAELEZWA UNA UHUSIANO WA KIMAPENZI
NA MSANII WA FILAMU, RIYAMA ALLY NA
UMEZAA NAYE. FAFANUA .
Hapana . Riyama ana maisha yake , ana
mwenzake na mtoto wake.
Kilichopo ni kwamba nipo naye karibu kikazi ,
halafu kwa bahati mbaya, jamaa yake na
Riyama anafanana sana na mimi , nadhani
watu wanashindwa kututofautisha .
LAKINI INASEMEKANA RIYAMA ALIKUPORA
MIKONONI MWA ROSE NDAUKA NA
UHUSIANO WAO SASA SI MZURI , KISA NI
WEWE. UNASEMAJE ?
Siyo kweli . Hata hivyo , sipendi
kumzungumzia Rose kwa sababu ana mtu
wake na kila mtu anajua . Siyo vizuri kusema
chochote
kilichotokea kati yangu na yeye wakati
uliopita .
UNAKUTANA NA CHANGAMOTO GANI
KWENYE ‘GAME ’?
‘ Sometimes’ wasanii hawataki kubadilika ,
unaweza ukamshauri abadilishe baadhi ya
vitu kwenye wimbo wake ili uwe wa tofauti
anakataa. Tatizo wanakariri .
Mfano; nakumbuka wakati natoa idea yangu
kuboresha wimbo wa Hakunaga wa Suma
Lee , hakunielewa. Ilifikia mahali
tukakorofishana studio , lakini mimi nilikuwa
natetea kitu kizuri.
Ona sasa , mwisho wa siku , ngoma imetoka
imekuwa mzuka. Jamaa amepiga shoo nyingi
sana. Ni kwa sababu alitoa kitu cha tofauti .
Sasa hivi wasanii kibao wanamuiga .
TAJA TOP 6 YAKO YA WASANII WA BONGO
FLEVA
Wa kwanza kabisa ni Lady Jaydee , huyu
mdada ni mkali. Ameanza zamani na mpaka
sasa hajachuja . Anajua muziki , amewekeza
kwenye
biashara na anajua anachokifanya .
Wengine ni Ben Pol, Vanessa Mdee, Diamond ,
Ali Kiba na AY. Hawa nawakubali sana. Wapo
kwenye nafasi za juu kwa upande wangu.
KUNA MADAI KUWA WASANII WA KIKE
WANA SHINDWA KUWIKA KWA SABABU
WAKIJA STUDIO MNAWATAKA KIMAPENZI,
IMEKAAJE HIYO ?
( Anacheka sana ) Kama wapo walio
kwamishwa kwa mtindo huo nadhani
wamejitakia wenyewe tu . Hivi msanii kama
amekuja kikazi,
utaweza kujiingiza kwenye mambo ya
kimapenzi ?
Utakuta msanii anakwenda studio , amevaa
kimitego halafu usiku ! Unategemea nini?
Hata sisi ni binadamu bana ( anacheka tena ) .

MR BLUE: WEMA , NAJMA WALINIFILISI


NYOTA wa Bongo Fleva , Herry Samir maarufu
kama Mr. Blue amesema wasichana
warembo , Wema Sepetu na Najma ambao
aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati
tofauti miaka ya nyuma , walimfilisi kutokana
na matumizi makubwa ya fedha alipotoka
nao viwanja.
Nyota wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu
kama Mr. Blue akiwa kwenye pozi.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni ,
Mr. Blue , msanii aliyeanza kupata umaarufu
akiwa bado kijana mdogo , alisema
alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao ,
kwani vinginevyo wangemuona hana pesa ,
kitu ambacho hakuwa tayari kuona
kinatokea.
“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana
starehe , kila day ( siku ) wanataka twende
kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka
niliyumba kimuziki .
Wema Sepetu a .k. a ' Beautiful Onyinye' .
“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani ,
ila kuna Wema na Najma , ilikuwa ukizama
nao dukani lazima ufanye shopping
( manunuzi ) ya nguvu, kuanzia laki saba,
nane na kuendelea ili wakuone unazo na
mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo,
sms hazikauki kuomba uwatumie mawe
( pesa ) , ” alisema .
Kuhusu maisha yake ya sasa , Mr. Blue
alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa
ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu
na amejaliwa kupata mtoto mmoja , hivyo ni
baba wa familia ambaye pia anakaribia
kumaliza mjengo wake siku si nyingi .
Mrembo Najma.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu , ana
malengo na upendo kwani amekuwa
akimuaga kila safari anayofanya na kwamba
hata yeye anaporejea nyumbani , hupokelewa
vizuri.
Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda
mrefu ambao bado wanafanya muziki na
wenye mashabiki wengi ndani na nje ya
Bongo.

Peter Wa P-square Aonyesha Jeuri Ya Pesa, Aonyesha Gari Yake Mpyaa Aliyonunua Kwa Zaidi Ya Milioni 300 Za Kibongo, Tazama Picha Hapa


Baada ya kumaliza matatizo yao kwenye familia
na ndugu zake ambayo bado hayajajulikana
kama yalikuwa ni kweli au ni stunt za biashara
yao kwenye muziki, Peter amewaonyesha fans
wake gari lake jipya lililomtoa zaidi ya milioni
300 kwenye pesa za kitanzania.
Peter na ndugu zake wawili ilisemakana
hawakuwa kwenye maelewano kwa kipindi kifupi
lakini baadae wote watatu wali-tweet maneno
ambayo yaliashiria wamemaliza tofauti zao.

Sketi yamtia mashakani polisi Kenya


Afisa Linda Okello akiwa kazini
Afisaa mmoja wa polisi mwanamke nchini Kenya
amepewa onyo kali kwa kuvalia sketi iliyokuwa
imembana kiasi cha kuonyesha umbo lake.
Wakuu wake walichukua hatua ya kumuonya
polisi huyo baada ya picha yake kusambazwa
kwenye mitandao ya kijamii na kupigiwa gumzo
kubwa.
Alipigwa picha akiwa amevalia sketi yake fupi na
yenye kumbana akiwa anashika doria katika eneo
ambako mashindano ya magari yalikuwa
yanafanyika eneo la Kati mwa Kenya.
Afisaa huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa
kufika mbele ya mkuu wake James Mugeria na
kuonywa vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara
nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni
utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya
heshima kwa polisi
Maafisa mjini Kiambu walisema kuwa kupewa
onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya
kuvalia sketi yake iliyokuwa imembana sana ni
jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa
kuendelea na majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa
kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti
moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake
kazini mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha
hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya
kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira
kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa
ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya
kumbana. Nini Kauli yako?

#BBC

JAY Z KUFANYA KUFURU KATIKA HONEYMOON YA BEST YAKE KANYE WEST

Jay Z ameripotiwa kumwambia rafiki yake wa
karibu kuwa yeye na mkewe Beyonce Knowles na
mtoto wao hawatahudhuria katika ndoa ya
swahiba wake Kanye West itakayofanyika mwezi
ujao jijini Paris Ufaransa.
Sababu za kutohudhuria ndoa hiyo zimeelezwa
kuwa ni kutokana na tukio hilo kupangwa
kuoneshwa kwenye reality show ya Keeping Up
with the Kardashians.
Hata hivyo, chanzo kimeliambia gazeti la The
Sun kuwa Jay Z amepanga kuwafanyia party
kubwa baada ya tukio hilo itakayofanyika New
York kwenye club yake ‘Club 40/40’ na kwamba
amepanga kutumia kiasi cha £100,000 katika
honeymoon yao kama zawadi yake.
“Instead he's making it up to his mate by
throwing him the most extravagant bachelor
party known to man. It will cost a small fortune
- and to top it all off, he's chucked a £100 000
yacht rental in there as a wedding gift as well.”
Kimeeleza chanzo hicho katika maelezo yake

KAJALA ATISHIA NA BUSINESS CLASS!WEMA AJIBU MAPIGO!

Ongeaza. Minenoooo

BEEF JIPYA JACK WOLPER NA AGNES MASOGANGE

Agness Masogange ambae aliwahi kutolewa
barua ya uchumba na Muhindi huyo mapema
mwaka huu, hata hivyo haikufahamika mambo
hayo yaliishia wapi.
Msanii Wolper akiwa na Prence Kass maarufu
kama Muhindi wa Masogange hapa nyota huyo
akionekana akiwa amelewa uso unamajibu kwani
hilo sio pozi la kawaida la mdomo kuubetua
kiasi hicho.
Na Sakina Shabani
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Xdeejayz
imenasa picha za msanii nyota wa filamu za
Kibongo Jackline Wolper akiwa na
mfanyabishara mmoja wa kihindi mwenye pesa
ndefu aliyefahamika kwa jina la Prence Kass
maarufu kama Muhindi wa Masogange.
Picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa
kwenye moja ya viunga vya Club ya usiku iliyopo
Oysterbay/ Masaki ambapo hata hivyo uhalisia
wa picha hizo unamuonesha Wolper akiwa bwii
kiasi cha kuubetua mdomo wake ambapo sio
kawaida kwa mtu mwenye ufahamu na staa
kama yeye kupiga picha zenye pozi baya kama
hizi.
Prence Kass ambae aliwahi kumchumbia Agness
Masogange hadi kwa mjombaake na msichana
huyo anawafunika mastaa wote bongo kwa
makalip yake tata na kila kitu kilikuwa kinaenda
swa kuhusu suala la kumuoa kwani Prence
alishamtengea zaidi ya milioni 40 ili
kumuachisha na mambo ya sanaa ili amfungulie
maduka.

MCHUNGAJI AWAOMBEA MACHANGUDOA ILI WAPATE WATEJA

Mchungaji Clement Kariuki wa
Yesu Ndani ya huduma makazi
katika barabara yenye
shughulinyingi ya River Road ni hasa
kwa kulenga wafanyakazi wa
ngono. Kwa mujibu wa matangazo
yake Billboardkujengwa nje ya
kanisa lake, mchungaji anaomba kwa
ajili ya makahaba kupata
wateja zaidi na kufanyafedha zaidi na
kuwafundisha jinsi ya kuwa
na kimaadili haki
katika biashara. Kanisa ambayo
inafanya kaziusiku tu kati ya 8
na 10:00 hadi sasa kuvutia zaidi ya
300 ya
waaminifu "i imani mchungaji na
kuaminiwakati anaomba me i
wanaweza kupata wateja zaidi kulala
na na kutengeneza
pesazaidi, kama yake kanisa yoyote."
alisema Mwende prostitue wakati
akizungumza na Nairobi wazi.
HAYA NI MJANGA KWA KWELI

DENTI AFIA KWA HAWARA


MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa
miaka 20 , mwanafunzi wa Chuo cha Eden
Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha
mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani
kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake,
Hafidh Mohammed .
Mwili wa Atu ukiwa chumbani kwa mtu
anayesadikika kuwa ni mpenzi wake, Hafidh
Mohammed.
Tukio hilo lilitokea April 26 , mwaka huu na
kukusanya umati huku mwanaume aliyelala
na binti huyo akitokomea
kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa
mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha ,
mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa
eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye
alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi
kulipokucha na kabla ya hapo , hakuwa
akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na msichana huyo kwa vile
aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke
mwingine ambaye alizaa naye .
“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu
ya uhusiano wao na huyu mwanafunzi ,
nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu
huku akionekana kuchanganyikiwa ,
nimejaribu kumsihi asikimbie lakini
imeshindikana,” alisema mama huyo.
Mwili wa Atu ukiingizwa kwenye gari la
polisi .
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha
masomo ya biashara na habari ambao
walikataa kutaja majina yao waliliambia
gazeti hili kuwa , marehemu Atu aliwaaga
anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza
wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya
Amana, Aprili 23, mwaka huu .
Hata hivyo , walisema uondokaji wake uliwapa
maswali mengi kwani tofauti na
walivyotegemea kuwa angebeba mfuko
mkubwa wenye nguo za kubadili , yeye
aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi
pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali .
Walisema siku tatu baadaye walipatwa na
mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli
yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao
kilichotokea katika chumba cha mvulana
huyo anayeishi jirani .
MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili
walisema kwao haikuwa mara ya kwanza
kumuona msichana huyo, kwani mara kwa
mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia
ndani hakuwa akitoka nje .
Walisema mara zote hizo , mwanaume huyo
mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na
kwenda kumnunulia chakula .
Wananchi na wanausalama wakiwa eneo la
tukio .
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA
TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na
kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani
ukiwa hauna jeraha , lakini pembeni yake
kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika
ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa
pamoja na mkoba wake hadi kituonis.
Minong ’ ono kutoka kwa majirani kuhusiana
na vidonge hivyo ilitofautiana , baadhi yao
walisema huenda vilitumika katika jaribio la
kutoa mimba , wengine walisema
inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa
wa ghafla usiku na mwanaume huyo
alikwenda kumchukulia vidonge hivyo
ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu
kupata nafuu .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani , SACP
Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kusema juhudi za kumtafuta
mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari
nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini
chanzo cha kifo hicho.

SIRI YA KUFUKUZA UZEE WA HARAKA


ENZI za uhai wake, marehemu Dk . Remmy
Ongalla aliwahi kuimba hivi : “Nikikumbuka
uzee huwa silali ”. Mungu ailaze roho yake
mahali pema peponi na tutaendelea
kumkumbuka daima . Wakati uzee ni ‘ tunu’ ya
maisha marefu toka kwa muumba, Dk .
Remmy alikuwa halali akiukumbuka tu kwa
kuwa uzee ni msururu wa matatizo mengi
lakini kubwa ni ya kiafya .
Ikumbukwe kuwa kila tukijiangalia
makunyanzi usoni ndiyo tunahisi hali ya uzee
bila kujua hata moyo, mapafu, ubongo , misuli ,
macho n.k . navyo huwa vimechakaa hivyo
kumfanya mzee aishi maisha tegemezi kwa
kila kitu .
Lakini upo uwezekano tena mkubwasana wa
kuufukuza uzee . Uzee hufukuzwa kwa njia ya
vyakula kwa kuchelewesha mchakato wa
mwili kujizeesha .
Ieleweke kuwa mwili wa binadamu ukipata
virutubisho sahihi basi seli za mwili
huboreshwa na mtu hunawiri na kuonekana
kijana hata kama ni mzee . Seli za mwili ndizo
zinazoungana kujenga mwili wa binadamu na
seli hizi zipo hai lakini zinahitaji lishe sahihi
ili ziwe na nguvu inayohitajika .
Seli hizi mara kwa mara hufa na mwili
hutengeneza seli nyingine kufidia zilizokufa
kila baada ya muda fulani. Mwili unaweza
kufidia seli zilizokufa kwa kuzalisha zingine
mpya ambazo zinaweza zikawa ni za aina
moja kati ya hizi tatu :
Ya kwanza ni seli zisizo na nguvu kama
zilizokufa. Seli hufa pale zinapokosa
virutubisho sahihi . Seli zinapokufa hufanya
mwili kuchoka na kuchakaa mapema na
hivyo kumfanya mtu aonekane mzee kuliko
umri wake. Hii kitaalamu huitwa “Body
Degeneration ”.
Aina ya pili ya seli ambazo mwili unaweza
kuzalisha kufidia zilizokufa ni zile ambazo
zitazalishwa nyingine lakini zitalingana ubora
na seli zilizokufa . Aina hii ya uzalishaji seli
huufanya mwili usinawiri na kubaki katika
hali ileile. Upatwapo na maradhi utajikuta
ukirudia dozi kadhaa bila kupona kwa kuwa
mwili huwa umedumaa . Haubomoki wala
haunawiri . Hii kitaalamu huitwa “Chronic
Condition ”.
Aina ya tatu ya seli zinazoweza kuzalishwa
kufidia zilizokufa ni seli zenye ubora na nguvu
kuliko zile zilizokufa. Katika hali hiyo ni
rahisi sana mzee kuonekana kijana kwa kuwa
seli mbovu hufa na huzalishwa seli bora na
imara kushika nafasi ya zilizokufa .
Hii kitaalamu huitwa “Body Regeneration ” na
ndiyo hufukuza uzee ( Anti- ageing Process ) .
Unaweza ukajiridhisha kwa macho tu kama
utafuata taratibu za mlo wenye nguvu za
kuufukuza uzee . Ila, hutakiwi uwe na haraka
ya matokeo wala usitegemee miujiza ya
kuamka na kupata mabadiliko .
Zingatia kila siku ulaji wa vyakula vyenye
asili ya majani na matunda katika kila mlo
wako kwa asilimia 75, huku ukiishinda hulka
ya mdomo kupenda vyakula vitamu visivyo
na tija mwilini .

WAKUBWA TU !!!..JE WAJUA NINI HUSABABISHA HAMU YA KUFANYA MAPENZ KILA MARA , SOMA HAPA


Kuna mambo mengi sana ambayo husabisha
kuhisi hamu ya kuwa na mwanaume au
mwanamke kila mara hapa nitaorodhesha
machache yale ya muhimu.
1) Upweke mara nyingi hupelekea sana akili ya
mtu kuhama na kutafuta kitu mbadala cha
kuweza kujiliwaza na mara nyingi huchagua raha
za kimwili kama kufanya mapenzi au kuwa na
mwenza karibu.
2) Story za Mapenzi kama vile kusoma vitabu vya
mapenzi kuangalia picha zenye mvuto wa
kimahaba pia kusikia habari hizo vyote hivi
vinaweza kukusababishia hamu kubwa sana ya
kufanya mapenzi.
3) Kuzoea sana kufanya tendo hilo na mtu
ambaye uko karbu nae, na kisha mtu huyo
kuondoka au kutenga nae, hii hali inaweza kukupa
shida sana kwani huduma ya karibu tena hauna
hivyo utaishia tu kuwa na hamu sana ya tendo
hilo na kuanza kuhangaika kutafuta njia
mbadala.
4) Pombe na vilevi vingine pia huleta sana hamu
ya tendo la ndoa wakati mwengine watu hufikia
hata kubaka kwa kushindwa kujizuia.
Haya ndio machache makubwa yanayoweza
kusababisha mtu kupatwa na hamu ya tendo a
ndoa mara. Unaweza kuyaepuka...!!?

DIAMOND ANATAFUTWA CHINA .....ALIYEJIFANYA DANSA WAKE ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA


STAA wa muziki wa bongo fleva nchini,
Abdul Nassib "Diamond" ametakiwa
kutokanyaga kabisa nchini China na
kwamba akitokeza pua yake nchini
humo asahau kabisa kurudi uraiani...
Hiyo inafuatia kijana mmoja mtanzania
kukamatwa wiki iliyopita uwanja wa
ndege wa Macau China na kudai kuwa
yeye ni mcheza shoo wa mwanamuziki
Diamond kutoka Tanzania....
Habari kutoka Macau China zinadai
kuwa kijana huyo aliyejulikana kwa jina
moja la Manyota alikamatwa akiwa
kwenye harakati za kuingiza mzigo huo
wa dawa za kulevya kwa kupitia
uwanja wa ndege wa Macau..
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya
habari, inaarifiwa kuwa Manyota
alikamatwa Alhamisi ya wiki iliyopita
katika uwanja uleule aliokamatwa
mtanzania mwingine Jackline Patrick,
anayesotea rumande mpaka hii leo huko
huko Macau China.
Kijana mmoja wa kitanzania anayefanya
shughuli zake huko China amedai kuwa
Manyota alikamatwa na maofisa wa
usalama wa uwanja wa ndege na katika
utetezi wake alidai kuwa yeye ni
mwanamuziki toka Afrika Mashariki...
Mtanzania huyo aliendelea kudai kuwa,
Manyota baada ya kukamatwa alianza
kubabaika kwa kujifanya mwanamuziki
na baadae akadai kuwa yeye ni mcheza
shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania....
"Alijifanya yeye ni mwanamuziki, baadae
akabadilika na kudai yeye ni mcheza
shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania na kwamba ndani ya ule
mzigo alikuwa hajui kuna nini zaidi ya
kuombwa na jamaa zake wa Dar
awapelekee nchini China"...Alisema
mtanzania huyo
Inasemekana kuwa, ili kujiridhisha,
maofisa hao wa usalama wa uwanja wa
ndege walimtaka kijana huyo aoneshe
moja ya kazi zake na yeye akaishia
kuwaonesha moja ya video za Diamond
kupitia mtandaoni na kumuonesha
mmoja wa wacheza shoo wa
mwanamuziki huyo kuwa ndo yeye
Manyota...
Inasemekana kuwa, pamoja na utetezi
wake huo ambao unaweza kumuingiza
matatani Diamond,maofisa hao wa
usalama walishndwa kumuelewa na
kumtupa ndani.....
Mtanzania huyo alihitimisha kwa kudai
kuwa, kutokana na mazingira yalivyo,ni
vyema mwanamuzi Diamond akawa
makini sana kama atakuwa na safari
za kwenda China kwani kwa namna
moja ama nyingine jina lake limewekwa
kwenye orodha ya majina machafu na
wanaweza kumkamata kwa lengo la
kuujua ukweli... .

NAY WA MITEGO ASAKWA KWA KUTISHIA KUUA


KIMENUKA! RB namba KT/RB/1178 /2014 -
KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO
inamsaka staa wa Ngoma ya Nakula Ujana ,
Emmanuel Elibariki ‘ Nay wa Mitego ’ kwa
tuhuma ya kutishia kumuua mdogo wake
aliyetajwa kwa jina la Amani Shija, Ijumaa
Wikienda limeinyaka .
Staa wa Ngoma ya Nakula Ujana , Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ .
Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa
akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano
nyumbani kwake, Manzese jijini Dar .
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na
Shija ulianza zaidi ya miezi mitatu iliyopita
ambapo hivi karibuni walikuwa maeneo ya
Kijitonyama, Dar , wakipata chakula cha usiku
na marafiki zao wengine ndipo ghafla dogo
akajichanganya na kujikuta akiropoka neno
lililomuudhi Nay , akapaniki .
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki , Nay
alianza kumfokea Shija na kutishia kumuua ,
ambaye alishindwa kujizuia na kujikuta
akimwaga chozi .
Akaendelea kueleza kuwa hata baada ya siku
hiyo , Nay aliendelea kumtumia SMS za
kutishia kumuua ambazo bado anazo kama
ushahidi Baada ya kudaka mchongo huo ,
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija ambaye pia
ni msanii wa Bongo Fleva na kumuuliza juu
ya malalamiko hayo, akakiri kugombana na
kaka yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay
amekuwa akiendelea kumtishia kumuua
jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Alisema ili kujilinda ndipo alipoamua
kulifikisha suala hilo kwenye Kituo cha Polisi
Kitunda, Dar anakoishi kwa sasa kisha
kufunguliwa jalada la kesi namba KT/
RB/1178 /2014 KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA
MTANDAO .
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila mafanikio lakini
kwa mujibu wa mtu wake wa karibu , baada
ya kujua msala huo ametorokea nchini China .

MAMA LORAA AINGILIA KATI PENZI LA ISABELA , KALAMA!


MAMA mlezi wa wasanii wa filamu Bongo,
Catherine Ambakisye ‘ Mama Loraa’
ameingilia kati penzi la wasanii wawili,
Isabela Mpanda na Luteni Kalama lililovunjika
na kuwapatanisha .
Wasanii wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda na
Luteni Kalama wakiwa katika pozi.
Isabela amethibitisha kuwa ni kweli
wamewekwa kiti moto na Mama Loraa
ambapo walikubali kurudiana na kudai ni
onyo la mwisho kwa Kalama na kama
atarudia tabia za ‘ kuchepuka ’ , ataachana
naye kabisa .
Isabela Mpanda.
“Namshukuru mama Loraa maana anatamani
kuona ninaoana na Kalama na kwa sababu
tumeshakaa muda mrefu kwenye uhusiano ,
yupo tayari hata kugharamia ndoa yetu , ”
alisema Isabela.

FLORA AFUNIKA KWA MAUNO


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Flora
Mvungi amenaswa akiwafunika vibaya
mastaa wenzake kwa kunengua .
Mwigizaji wa sinema za Kibongo , Flora
Mvungi .
Mpambano huo usio rasmi ulichukuwa nafasi
wiki iliyopita katika Ukumbi wa New Maisha ,
Masaki jijini Dar ambapo kulikuwa na shoo
maarufu kwa jina la Bunyerobunyero .
Flora alipoulizwa na mwanahabari wetu juu
ya ufundi huo wa kucheza Kibao Kata
kilichokuwa kikipigwa na kuwazidi mastaa
kama Kajala Masanja , Zuwena Mohamed
‘ Shilole’ na Halima Haroun ‘ Kimwana ’ ,
hakuwa tayari kujibu zaidi ya kuendelea
kukatika.

BATULI AKUBALI KUIGIZA NUSU UTUPU


MWANADADA mkali wa Bongo Movies ,
Yobnesh Yusuph ‘ Batuli’ amefunguka kuwa
kwa sasa yupo tayari kuigiza nusu utupu kwa
sinema za nje ya nchi .
Mwanadafada mkali wa Bongo Movies,
Yobnesh Yusuph ‘ Batuli’.
Akipiga stori mbili- tatu na kona hii , Batuli
alisema kuwa muvi nyingi Bongo huwa
zinafungiwa kwa kukosa maadili na kwamba
kama ikitokea nafasi akaitwa nje ya nchi
kuigiza sini hizo , atakuwa tayari.
“Zamani nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu
utupu. Wenzetu Nigeria wameendelea na
ndiyo maana wanaigiza hata nusu utupu ,
kama itatokea nafasi ya kuigiza huko ( nje ya
Bongo) nusu utupu, nipo tayari, ” alisema
Batuli.

JOKATE, NATURE WATIFUANA!


PASUA jipu! Mastaa wawili wenye majina
makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate
Mwegelo ‘ Kidoti ’ na Mbongo- Fleva Juma
Kasim ‘ Juma Nature ’ wanadaiwa kuacha
mshangao kwa wasanii wenzao baada ya
kutifuana, Ijumaa Wikienda limeng’ atwa sikio .
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘ Juma
Nature ’.
Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga
kutomaindi lakini habari za kushangaza
zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke
amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo
kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya
ndala au kandambili .
Kabla ya madai haya mapya , Nature aliwahi
kunukuliwa redioni wakati akitambulisha
wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa
yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni .
Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature
amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘ amekopi’
na ‘ kupesti’ wazo lake la biashara .
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti ’.
Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa
akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa
bila mafanikio .
“Nature amekuwa akimpigia simu Jokate
lakini haipokelewi, ” kilidai chanzo hicho kwa
sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu
wa bastola .
Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika
kuziona kandambili za Jokate lakini
amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa
mrembo huyo kamuibia .
NATURE AFUNGUKA
Alifunguka : “Hadi sasa hivi sijabahatika
kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu
wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo
langu.
“Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao
sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu
mbaya.
“Kweli sikutegemea kama ishu kama hiyo
ingefanywa na mtu kama yeye ( Jokate ) ila
hata kama ametoa mimi wazo langu liko
palepale .“Nitakuja kuzitoa tu hizo kandambili
zenye picha na jina langu. ”
Kandambili zilizosababisha mtifuano .
BOFYA HAPA KUMSIKIA JOKATE
Baada ya kusikia upande mmoja wa Juma
Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa
habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na
kumsomea mashitaka yake hayo ya kuiba
wazo la biashara la Juma Nature .
Bila kupepesa macho wala kuchezesha
masikio , Jokate alifunguka kwamba kwa
upande wake anasikitishwa na mtu kama
Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu
anaowaheshimu.
Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza
kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake .
“Wewe siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo
kutoka kwa Nature , niliamini baada ya mimi
kutoa hizo ndala , atanisapoti kwani mimi
niko katika kuendeleza na kutoa ajira kwa
vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu
letu la maisha .
MASIKITIKO
“Kweli Nature amenisikitisha sana kwa
kitendo chake cha kunitangazia ubaya.
“Hata hivyo , siwezi nikaacha kutoa bidhaa
zangu, nitaendelea kutoa ‘ so ’ itabidi tu
anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za
kwake,” alisema Jokate, mmiliki wa lebo ya
mavazi ya Kidoti.
MASTAA WANASEMAJE KUHUSU SAKATA
HILO ?
Wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya
mastaa ambao walionesha kushangazwa na
sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na
Nature kuhitilafiana wakati kazi zao
zinategemeana .
“Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo
tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni
watu ambao muda wowote wanaweza
kukutana kwa ajili ya kufanya kazi , ” alisema
mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Bongo
Fleva .
NATURE KAMGEUKA JOKATE ?
Kwa mujibu wa mastaa hao, awali Nature
aliposikia Jokate ana ‘ aidia ’ kama hiyo
alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii
mwenzake hivyo kipato atakachopata
kitamsaidia maishani lakini kumbe
inawezekana kimoyomoyo ilimuuma ndiyo
maana ameendelea kumtuhumu Jokate.
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Ni vyema Jokate na Nature wakakaa na
kukubaliana waifanye biashara hiyo kwa
pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa
zaidi , ni kiasi cha kuona fursa na kuitumia .

SOMO SAHIHI LA KUPUNGUZA MAWAZO NA KUONGEZA FURAHA!


MUELEZE HUJISIKII VIZURI
Ikibidi sema unaumwa . Mpenzi bora
atapunguza maswali au baadhi ya vitu na
kukuacha upumzike . Hiyo itakusaidia
kuingiza hewa kichwani ambayo
itakuongezea nafasi na mwisho kichwa
kitakuwa chepesi.
Maneno ya hapa na pale ukiwa na msongo
wa vitu kichwani , utaona kama ni vuvuzela
zinapulizwa masikioni . Unapomuomba
mwenzio akupe nafasi ya kupumzika kwa
sababu hujisikii vizuri, itakusaidia kupunguza
uzito wa kichwa .
ANGALIZO ;
Unapaswa kuwahi kujieleza kabla mwenzako
hajaanza yake, kwa maana akisema yeye
halafu wewe ndiye ufuate, atajua umeamua
kumkwepa .
LALA USINGIZI
Tafuta usingizi kisha utokomee kwenye njozi ,
ukiamka hutokuwa yule yule . Angalau kichwa
kitakuwa kimepumua na uzito umepungua.
MUELEZE KINACHOKUSUMBUA
Ni tiba kwako endapo utafungua kinywa na
kumueleza mwenzio kile ambacho
kinakusumbua. Atajua kinachokusibu , kwa
hiyo atajua jinsi ya kukuzoea kuliko kufika na
kukaa kimya au kumjibu mkato au kufoka bila
mpango.
CHAGUA KINACHOKUFURAHISHA, FANYA
Unapenda kungalia filamu au kingine
chochote na unaamini ukikifanya
kitakuondolea hasira , basi fanya ili kujiweka
vizuri kisaikolojia mbele ya mwenzi wako .
Kuna wale ambao hasira zao hutoweka
baada ya kupanda kitandani , nalo si tatizo
ilimradi kutibu hasira .
Angalizo ni kwamba kupanda kitandani
kunahitaji uhuru wa hisia . Utazungumza vipi
na mwenzi wako mpaka mkubaliane kupeana
hiyo dawa? Muhimu ni kumueleza
kinachokusibu , akikuhurumia, basi huo ndiyo
uwe mwanzo wa kutii kiu .
UVUMILIVU
Yote ni muhimu lakini uvumilivu ni kitu cha
msingi. Jifunze kusikiliza vitu bila kutoa
majibu. Acha baadhi ya mambo yawe fahari
ya masikio . Inawezekana umesikia na jibu
unalo lakini unatakiwa uitambue hali
uliyonayo , kwa hiyo endelea kunyamaza .
Ukiweza hili basi umefaulu mtihani mgumu
na haitatokea ugombane na mwenzio kisa
umeudhiwa kazini kwako au kwenye
daladala.
HITIMISHO
Zingatia hayo ambayo nimekudokezea
mwanzo mpaka mwisho . Hivyo ndivyo
unavyoweza kuongeza furaha yako na
kupunguza mawazo. Nakusisitiza kupiga vita
msongo wa mawazo kwa sababu mara nyingi
hupoteza njia. Mhusika hukosa mwanga wa
kupata ufumbuzi .
Unapokosa ufumbuzi , itakusababishia
kufanya uamuzi ambao siyo sahihi , hivyo
kukuelekeza kwenye majuto ya baadaye.
Hakuna sababu ya kujuta , shughulikia
mambo yako kwa utaratibu . Makala haya ni
dira yako katika kukupunguzia mawazo na
kukuongezea furaha.

MTANGAZAJI JERRY MURO YUPO WAPI ?


Hivi mwandishi huyu yupo wapi kwa sasa? au
ndio ameshamalizwa na kufifishwa katika
shughuli zake za uandishi? Ninapenda kujua toka
kwenu wadau, nini kinaendelea.

Irene Uwoya Aingia Katika Bifu na Frola mvungi Baada Ya Kusema H-baba Hajui Chochote Katika 6 Kwa 6


Uwoya amchana live mpenzi wa Flora Mvungi i.e
H-baba kwamba hafai katika mapenzi kwa
sababu hana stamina katika uwanja wa 6 kwa 6.
Flora Mvungi naye akaja juu na kudai kwamba
maneno ya Uwoya ni maneno ya mkosaji na
akadai zaidi kwamba H-baba hana tatizo katika
mapenzi na yuko fiti ile mbaya.
Wakati malumbano yakiendelea,dada mmoja
akapiga simu clouds fm,akakataa kutaja jina lake
lakini naye akazidi kuchagiza kwamba H-baba si
lolote si chochote katika ulingo wa ma-lovey
dovey,ana mbwembwe za kukata viuno jukwaani
tu.Haya ndio mapenzi ya ma-star wa ki-bongo.

HAMISA MABETO AWATISHIA AMANI WASANII WA KIKE BONGO MOVIES


MWANAMITINDO maarufu nchini, Hamisa
Mabeto ametishia maslahi ya wasanii wa kike
wa Bongo Movie baada ya kujitosa rasmi
kwenye tasnia hiyo na kung’ara katika Filamu ya
VIP akiwa na mastaa, Vincent Kigosi ‘Ray’ na
Jacqueline Wolper.
“Wasanii wajiangalie nafasi zao baada ya
Mabeto kuingia kwenye filamu maana ndani ya
VIP amekamua sana na wasipokuwa makini
atawasumbua kutokana na mvuto ulionao,”
alisema Ray.
Mabeto ametamba kwenye ulimbwende tangu
mwaka 2010 alipoibuka mshindi wa shindano
XXL Back to School Bash.
Mwaka 2011 alishika nafasi ya pili katika
shindano kumsaka Miss Dar Indian Ocean na
baadaye Miss Kinondoni.
Mwaka 2011 alishiriki Miss Tanzania na kufika
hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Mwaka
2012 akafika hatua ya kumi bora kwenye Miss
University.
Hivi karibuni alipata ulaji wa kupamba kava la
gazeti moja la Kenya.

TOM & JERRY..MTWARAAAA MOJA GET READY!


Wakazi wa kusini mwa Tanzania yaani mkoa wa
Mtwara wametakiwa kukaa mkao wa kula
burudani ya nguvu ya muziki itapigwa moja
kwa moja jukwaani siku ya tarehe 2 ya mwezi wa
Mei katika ukumbi wa Makonde Club.
Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na
si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo
flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya
Mashariki kwa sasa kupitia vibao vyake vitamu
kama vile cha My Number One remix
alichomshirikisha msanii Davido kutoka nchini
Nigeria, Raisi wa wasafi ama Diamond
Platinumz”Asali ya warembo”kama mashabiki
wake wanavyomwita.
Mwanamuziki Diamond atafanya shoo laivu
mkoani Mtwara chini ya udhamini mkubwa wa
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
akisindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo
Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’
au Madame kama mashabiki
wake wanavyopenda kumwita.
Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye
mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa
ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje
ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na
hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa
kuwania tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika.
Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na
shoka kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twissa amebainisha kuwa tukio
hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya burudani
kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na
kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia
huduma zetu.
“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini
kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya
Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom
imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa
na kwa kipindi chote hicho watanzania
wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya
tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano
nchini,” alisema Twissa.
Kwa kuongezea Twissa amewataka wakazi na
mashabiki wote wa Diamond na muziki wa Bongo
Flava kujitokeza kwa wingi kwani mbali na
burudani kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali
mbali za Vodacom.
Katika kunogesha shoo hiyo kwa wakazi wa
kusini Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema
Sepetu naye akasema haitokuwa poa kama
asipomsindikiza asali wake wa moyo kwenda
kujivinjari pande hizo na mashabiki wao. Kwa
tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara wanabahati
kubwa ya kutembelewa na mastaa wawili
wakubwa kutoka tasnia mbili tofauti nchini.
“Hii shoo si ya kukosa kabisa kwani hakuna
kiingilio bali ni uwepo wako tu na kujiandaa
kwako kwa burudani ndio kinachohitajika.
Tunawapenda sana wateja wetu wa Mtwara,
hatuna uwezo wa kulipa kutokana na kuwa
wateja wetu waaminifu siku zote lakini ninaamini
kwa pamoja tunaweza kujumuika na kufurahia
wakati tulionao. Naombeni mjitokeze kwa wingi,
rafiki amlete rafiki yake ili tuwe pamoja
siku hiyo.”