TOM & JERRY..MTWARAAAA MOJA GET READY!


Wakazi wa kusini mwa Tanzania yaani mkoa wa
Mtwara wametakiwa kukaa mkao wa kula
burudani ya nguvu ya muziki itapigwa moja
kwa moja jukwaani siku ya tarehe 2 ya mwezi wa
Mei katika ukumbi wa Makonde Club.
Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na
si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo
flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya
Mashariki kwa sasa kupitia vibao vyake vitamu
kama vile cha My Number One remix
alichomshirikisha msanii Davido kutoka nchini
Nigeria, Raisi wa wasafi ama Diamond
Platinumz”Asali ya warembo”kama mashabiki
wake wanavyomwita.
Mwanamuziki Diamond atafanya shoo laivu
mkoani Mtwara chini ya udhamini mkubwa wa
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
akisindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo
Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’
au Madame kama mashabiki
wake wanavyopenda kumwita.
Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye
mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa
ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje
ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na
hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa
kuwania tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika.
Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na
shoka kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twissa amebainisha kuwa tukio
hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya burudani
kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na
kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia
huduma zetu.
“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini
kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya
Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom
imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa
na kwa kipindi chote hicho watanzania
wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya
tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano
nchini,” alisema Twissa.
Kwa kuongezea Twissa amewataka wakazi na
mashabiki wote wa Diamond na muziki wa Bongo
Flava kujitokeza kwa wingi kwani mbali na
burudani kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali
mbali za Vodacom.
Katika kunogesha shoo hiyo kwa wakazi wa
kusini Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema
Sepetu naye akasema haitokuwa poa kama
asipomsindikiza asali wake wa moyo kwenda
kujivinjari pande hizo na mashabiki wao. Kwa
tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara wanabahati
kubwa ya kutembelewa na mastaa wawili
wakubwa kutoka tasnia mbili tofauti nchini.
“Hii shoo si ya kukosa kabisa kwani hakuna
kiingilio bali ni uwepo wako tu na kujiandaa
kwako kwa burudani ndio kinachohitajika.
Tunawapenda sana wateja wetu wa Mtwara,
hatuna uwezo wa kulipa kutokana na kuwa
wateja wetu waaminifu siku zote lakini ninaamini
kwa pamoja tunaweza kujumuika na kufurahia
wakati tulionao. Naombeni mjitokeze kwa wingi,
rafiki amlete rafiki yake ili tuwe pamoja
siku hiyo.”

0 comments:

Post a Comment