HAMISA MABETO AWATISHIA AMANI WASANII WA KIKE BONGO MOVIES


MWANAMITINDO maarufu nchini, Hamisa
Mabeto ametishia maslahi ya wasanii wa kike
wa Bongo Movie baada ya kujitosa rasmi
kwenye tasnia hiyo na kung’ara katika Filamu ya
VIP akiwa na mastaa, Vincent Kigosi ‘Ray’ na
Jacqueline Wolper.
“Wasanii wajiangalie nafasi zao baada ya
Mabeto kuingia kwenye filamu maana ndani ya
VIP amekamua sana na wasipokuwa makini
atawasumbua kutokana na mvuto ulionao,”
alisema Ray.
Mabeto ametamba kwenye ulimbwende tangu
mwaka 2010 alipoibuka mshindi wa shindano
XXL Back to School Bash.
Mwaka 2011 alishika nafasi ya pili katika
shindano kumsaka Miss Dar Indian Ocean na
baadaye Miss Kinondoni.
Mwaka 2011 alishiriki Miss Tanzania na kufika
hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Mwaka
2012 akafika hatua ya kumi bora kwenye Miss
University.
Hivi karibuni alipata ulaji wa kupamba kava la
gazeti moja la Kenya.

0 comments:

Post a Comment