Paul Okoye azilaumu media za Naija kwa kuukuza ugomvi wao, ‘never underestimate the power of blood’


Baada ya mapacha wa P-Square na kaka yao
Jude Okoye kuthibitisha amani imerejea baina
yao, Paul Okoye amezitupia lawama media za
Nigeria kuwa zilikuza ugomvi wao ambao amedai
ulikuwa mdogo na wa kawaida.
“Ugomvi na mgogoro wa mapacha sio kitu
kikubwa ni vile tu Naija media waliukuza kupita
kiasi” alisema Paul.
Paul pia amemtetea mke wa pacha wake Peter
kuwa hakuhusika kwa lolote katika mgogoro wao
hivyo kuwaomba watu wasimlaumu Lola sababu
hana hatia.
Paul aliongeza kuwa watu wasichukulie poa
nguvu ya damu (ndugu) kwa kumaanisha kuwa
sio kitu rahisi kuwatenganisha.
Hiki ndicho alichokiandika Paul Okoye kupitia
ukurasa wake wa facebook jana:
Please whatever happen was not cause by any
woman, pls and pls stop blaming ma brother’s
wife Lola for wat she’s innocent. Twins fight and
quarrel is not a big deal only dat naija media
over-emphasized it, but never underestimate the
power of blood. It’s thicker than water. Much love
to y’all. #Family #ForeverPsquare
Wakati huo huo siku moja baada ya ndugu hao
kuthibitisha kuwa wameyamaliza matatizo yao,
Peter, Paul na Jude Okoye walionekana pamoja
juzi katika sherehe ya model aitwaye Sarah Ofili.

0 comments:

Post a Comment