MCHINA AJINYONGA BAADA YA KUBORONGA UJENZI WA DARAJA MOROGORO

Raia mmoja wa China ambaye ni mhandisi
katika Kampuni ya Ujenzi ya China Railway
Bureu 15 Group inayojenga Daraja la Mto
Kilombero, Qin Bao Feng amekufa kwa
kujinyonga kwa kile kinachodaiwa ni baada ya
kuboronga katika kazi.
Ilielezwa kuwa Feng aliamua kujinyonga baada
ya nguzo za daraja alilokuwa akilisimamia
katika ujenzi huo, kusombwa na maji, jambo
ambalo aliona kuwa limemvurugia kazi yake.
Baadhi ya watu waliokuwa jirani na kambi hiyo,
walisema baada ya kuharibika kwa kazi hiyo,
wahandisi wenzake kutoka China, walianza
kumtenga hali iliyomfanya ajione kuwa mpweke
na hatimaye kuchukua uamuzi huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro,
Leonard Paulo alisema tukio hilo lilitokea
Jumamosi iliyopita ndani ya kambi ya kampuni
hiyo.
Alisema mwili wa marehumu ulikutwa
ukining’inia kwenye dari ndani ya chumba
alichokuwa analala na kwamba polisi
wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio
hilo.
Kamanda Paulo alisema baada ya kuchunguza
mwili wa marehemu walikuta karatasi iliyokuwa
imeandikwa ujumbe kwa lugha ya Kichina.
Alisema kwa kuwa hakuna mkalimani aliyekuwa
jirani na eneo la tukio, polisi wanaendelea
kumtafuta mtu wa kuutafsiri.
Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo
umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis
iliyopo Kilakala, Morogoro.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

Post a Comment