BATULI ADAIWA KUITIKISA NDOA YA MTUNIS


HABARI za motomoto kutoka vyanzo vya
uhakika , zinasema kuwa staa wa kike
anayekuja juu kwa sasa katika tasnia ya
filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘ Batuli ’
ameitikisa ndoa ya mwigizaji mwenzake , Nice
Mohammed ‘ Mtunis ’ kwa madai ya kutoka
naye kimapenzi .
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo,
Yobnesh Yusuph ‘ Batuli’.
Chanzo chetu , kwa sharti la kutochorwa jina
lake gazetini kilifunguka kuwa ishu ya wawili
hao kuwa wapenzi siyo siri, kwani mara
kadhaa wamekuwa wakijiachia sehemu
mbalimbali , huku mke wa Mtunis
akinyetishiwa, jambo lililosababisha
migongano ndani ya ndoa hiyo .
“Mmechelewa kweli kujua! Leo ndiyo
mnauliza kuhusu Mtunis na Batuli? Hao ni
wapenzi na penzi lao limenoga kwelikweli
sasa hivi . Imefikia hatua Mtunis na mkewe
hawana maelewano mazuri . Nyumba ni kama
inayumbishwa na Batuli lakini Mtunis hataki
kumwacha Batuli, ” kilipasha chanzo hicho.
Mkongwe wa filamu za Kibongo , Nice
Mohammed ‘Mtunis ’.
MTUNIS KIKAANGONI
Kama ada , Risasi Mchanganyiko lina desturi
ya kupata mzani wa habari kabla ya
kuirusha, ndivyo ilivyofanyika kwa Mtunis
ambaye aliposomewa mashitaka yake
alipovutiwa waya , alikanusha vikali akidai
ndoa yake ina amani na hana uhusiano na
Batuli.
“Kwanza nani amekuambia kuwa mimi
natoka na Batuli? Yule ana mtu wake na
mimi nina ndoa yangu. Sikia kaka , katika
kipindi ambacho ndoa yangu ina amani ni
hiki , sitaki kabisa haya mambo . Mtakuja
kusababisha Batuli agombane na mumewe
kisa mimi ,” alisema Mtunis kwa sauti ya juu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA BATULI
Batuli alipopatikana kwa njia ya simu,
alikuwa msikivu muda wote alipoelezwa
kuhusu madai hayo , mwishoni akajibu kwa
mtindo wa kuuliza : “Kwanza nikuulize, Mtunis
ni Muislam au Mkristo?”
Mwandishi wetu alipomjibu kuwa ni Muislam,
akaendelea: “Sasa kipi cha ajabu hapo ? Kwa
imani yake ya Kiislam , ana ruhusa ya kuoa
wake hadi wanne . Halafu kuna wakati
nilishaishi naye miaka si chini ya minne, kwa
hiyo sioni ajabu hapo . Hata kama ikitokea
tena hakuna tatizo.
KUITIKISA NDOA YA MTUNIS
“Achana na watu bwana, acha tu watu
waongee . Lakini ninachosema hakuna cha
ajabu hapo. Maisha yanaruhusu, yaani
kisheria hata Mungu anaruhusu - siyo ajabu.
Siwezi kuzungumza zaidi maana nimesafiri
nipo kwenye harusi , dada yangu anaolewa .”

0 comments:

Post a Comment