ALIYEPIGWA NA CHID BENZ MAHUTUTI


MREMBO Mwanaisha Kiboye, mkazi wa Ilala,
Dar anayedaiwa kupigwa na mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Bongo, Rashid Makwilo ‘ Chid
Benz’ , hali imekuwa mbaya kwani yu
mahututi.
Mwanaisha Kiboye , akiwa hoi hospitali
baada ya kipigo kutoka kwa msanii Chid
Benz .
Juzi Jumatatu , wakati staa huyo
akipandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Wilaya ya Ilala, Dar kwa kesi hiyo ,
Mwanaisha alikuwa akipumua kwa tabu
kwenye chumba maalum katika Hospitali
iitwayo Aviation iliyopo maeneo hayo ya Ilala .
MAMA MDOGO ANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mama mdogo wa Mwanaisha
aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, hali
ya mgonjwa imekuwa tete kwani kwa siku
moja amekuwa akizimia zaidi ya mara tano.
Mtuhumiwa Chid Benz.
AZIMIA MARA TANO
“Mwanangu hali yake ni mbaya anazimia
zaidi ya mara tano kwa siku halafu watu
wananiambia nitoe kesi mahakamani si
nitaonekana chizi jamani ?” alisema mama
huyo huku akilengwalengwa na machozi.
Alisema hali ya mgonjwa imekuwa ikibadilika
hasa suala la presha kupanda na kushuka
huku mapigo ya moyo yakiwa chini hivyo
kuwatia hofu ndugu , jamaa na marafiki.
KIPIMO CHA KICHWA
Aliongeza kuwa siku hiyo ( Jumatatu)
madaktari na wauguzi walikuwa katika
harakati za kumpeleka kwenye kipimo
kiitwacho CT Scanning kuangalia madhara
yaliyompata kichwani na kusababisha hali
kuzidi kuwa mbaya .
Mwanaisha Kiboye akiendelea na matibabu
katika Hospitali ya Aviation, IIala.
Mwanahabari wetu alifanikiwa kuingia wodini
ambapo katika kipindi cha saa kadhaa
Mwanaisha hakugeuka wala kuamka kutoka
usingizini.
TURUDI KWENYE KESI
Juzi ( Jumatatu ) Chid alitakiwa kupandishwa
kizimbani Mahakama ya Mwanzo, Wilaya ya
Ilala, Dar kwa ajili ya kesi hiyo lakini
hakutokea kortini badala yake alimtuma
mdhamini wake amuombee udhuru kuwa
alikuwa akiumwa.
CHEMBA KIDOGO
Karani wa mahakama hiyo , Nusura Seleman
alipoita kesi hiyo , mdhamini huyo na ndugu
wa Chid Benz na ndugu wa Mwanaisha,
walijongea kwenye ‘ chemba kidogo’ mbele ya
Hakimu Leonia Muta .
HAIWEZEKANI
Katika kesi hiyo ambayo mwanahabari wetu
aliifuatilia hatua kwa hatua, hakimu Muta
aliwaita wenye kesi hiyo lakini wote
hawakuwepo ndipo hakimu huyo akasema
hawezi kuendelea na kesi hiyo bila wenye kesi
wote kuwepo . Shauri hilo liliahirishwa hadi
Mei 5, mwaka huu.
MAMA CHID ATOLEWA NDUKI
Akizungumza nje ya mahakama hiyo , kaka
wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina la
Swedy alisema :
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya namna ile
halafu wanatuambia tukayamalize nyumbani ,
hilo si jambo la kushangaza jamani ?
Mama yake Chid Benz alikuja nyumbani
kutaka kumuona mgonjwa tukamtoa nduki.
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya hivyo
asijekudhurika na jambo lolote akiwa
nyumbani kwetu ikaonekana tumemfanyia
kusudi .
CHID NAYE ATOLEWA BARU
“Hata Chid Benz mwenyewe naye juzi
( Jumamosi iliyopita ) alikuja na kutupigia
magoti naye tukamtoa baru, asitulee zake
kwanza hii siyo mara ya kwanza kumpiga
dada yangu kuna kipindi alimpiga kesi ilikuwa
Kituo cha Polisi cha Kilwa Road. ”
BADO HALI TETE
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni
Jumatatu jioni , bado hali ya Mwanaisha bado
ilikuwa ni tete .
Chid Benz alidaiwa kumpiga Mwanaisha Siku
ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu maeneo ya
Ilala, Dar .

0 comments:

Post a Comment