NAY WA MITEGO ASAKWA KWA KUTISHIA KUUA


KIMENUKA! RB namba KT/RB/1178 /2014 -
KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO
inamsaka staa wa Ngoma ya Nakula Ujana ,
Emmanuel Elibariki ‘ Nay wa Mitego ’ kwa
tuhuma ya kutishia kumuua mdogo wake
aliyetajwa kwa jina la Amani Shija, Ijumaa
Wikienda limeinyaka .
Staa wa Ngoma ya Nakula Ujana , Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ .
Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa
akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano
nyumbani kwake, Manzese jijini Dar .
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na
Shija ulianza zaidi ya miezi mitatu iliyopita
ambapo hivi karibuni walikuwa maeneo ya
Kijitonyama, Dar , wakipata chakula cha usiku
na marafiki zao wengine ndipo ghafla dogo
akajichanganya na kujikuta akiropoka neno
lililomuudhi Nay , akapaniki .
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki , Nay
alianza kumfokea Shija na kutishia kumuua ,
ambaye alishindwa kujizuia na kujikuta
akimwaga chozi .
Akaendelea kueleza kuwa hata baada ya siku
hiyo , Nay aliendelea kumtumia SMS za
kutishia kumuua ambazo bado anazo kama
ushahidi Baada ya kudaka mchongo huo ,
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija ambaye pia
ni msanii wa Bongo Fleva na kumuuliza juu
ya malalamiko hayo, akakiri kugombana na
kaka yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay
amekuwa akiendelea kumtishia kumuua
jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Alisema ili kujilinda ndipo alipoamua
kulifikisha suala hilo kwenye Kituo cha Polisi
Kitunda, Dar anakoishi kwa sasa kisha
kufunguliwa jalada la kesi namba KT/
RB/1178 /2014 KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA
MTANDAO .
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila mafanikio lakini
kwa mujibu wa mtu wake wa karibu , baada
ya kujua msala huo ametorokea nchini China .

0 comments:

Post a Comment