MAMA LORAA AINGILIA KATI PENZI LA ISABELA , KALAMA!


MAMA mlezi wa wasanii wa filamu Bongo,
Catherine Ambakisye ‘ Mama Loraa’
ameingilia kati penzi la wasanii wawili,
Isabela Mpanda na Luteni Kalama lililovunjika
na kuwapatanisha .
Wasanii wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda na
Luteni Kalama wakiwa katika pozi.
Isabela amethibitisha kuwa ni kweli
wamewekwa kiti moto na Mama Loraa
ambapo walikubali kurudiana na kudai ni
onyo la mwisho kwa Kalama na kama
atarudia tabia za ‘ kuchepuka ’ , ataachana
naye kabisa .
Isabela Mpanda.
“Namshukuru mama Loraa maana anatamani
kuona ninaoana na Kalama na kwa sababu
tumeshakaa muda mrefu kwenye uhusiano ,
yupo tayari hata kugharamia ndoa yetu , ”
alisema Isabela.

0 comments:

Post a Comment