DIAMOND ANATAFUTWA CHINA .....ALIYEJIFANYA DANSA WAKE ADAKWA NA MADAWA YA KULEVYA


STAA wa muziki wa bongo fleva nchini,
Abdul Nassib "Diamond" ametakiwa
kutokanyaga kabisa nchini China na
kwamba akitokeza pua yake nchini
humo asahau kabisa kurudi uraiani...
Hiyo inafuatia kijana mmoja mtanzania
kukamatwa wiki iliyopita uwanja wa
ndege wa Macau China na kudai kuwa
yeye ni mcheza shoo wa mwanamuziki
Diamond kutoka Tanzania....
Habari kutoka Macau China zinadai
kuwa kijana huyo aliyejulikana kwa jina
moja la Manyota alikamatwa akiwa
kwenye harakati za kuingiza mzigo huo
wa dawa za kulevya kwa kupitia
uwanja wa ndege wa Macau..
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya
habari, inaarifiwa kuwa Manyota
alikamatwa Alhamisi ya wiki iliyopita
katika uwanja uleule aliokamatwa
mtanzania mwingine Jackline Patrick,
anayesotea rumande mpaka hii leo huko
huko Macau China.
Kijana mmoja wa kitanzania anayefanya
shughuli zake huko China amedai kuwa
Manyota alikamatwa na maofisa wa
usalama wa uwanja wa ndege na katika
utetezi wake alidai kuwa yeye ni
mwanamuziki toka Afrika Mashariki...
Mtanzania huyo aliendelea kudai kuwa,
Manyota baada ya kukamatwa alianza
kubabaika kwa kujifanya mwanamuziki
na baadae akadai kuwa yeye ni mcheza
shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania....
"Alijifanya yeye ni mwanamuziki, baadae
akabadilika na kudai yeye ni mcheza
shoo wa mwanamuziki Diamond kutoka
Tanzania na kwamba ndani ya ule
mzigo alikuwa hajui kuna nini zaidi ya
kuombwa na jamaa zake wa Dar
awapelekee nchini China"...Alisema
mtanzania huyo
Inasemekana kuwa, ili kujiridhisha,
maofisa hao wa usalama wa uwanja wa
ndege walimtaka kijana huyo aoneshe
moja ya kazi zake na yeye akaishia
kuwaonesha moja ya video za Diamond
kupitia mtandaoni na kumuonesha
mmoja wa wacheza shoo wa
mwanamuziki huyo kuwa ndo yeye
Manyota...
Inasemekana kuwa, pamoja na utetezi
wake huo ambao unaweza kumuingiza
matatani Diamond,maofisa hao wa
usalama walishndwa kumuelewa na
kumtupa ndani.....
Mtanzania huyo alihitimisha kwa kudai
kuwa, kutokana na mazingira yalivyo,ni
vyema mwanamuzi Diamond akawa
makini sana kama atakuwa na safari
za kwenda China kwani kwa namna
moja ama nyingine jina lake limewekwa
kwenye orodha ya majina machafu na
wanaweza kumkamata kwa lengo la
kuujua ukweli... .

0 comments:

Post a Comment