Sketi yamtia mashakani polisi Kenya


Afisa Linda Okello akiwa kazini
Afisaa mmoja wa polisi mwanamke nchini Kenya
amepewa onyo kali kwa kuvalia sketi iliyokuwa
imembana kiasi cha kuonyesha umbo lake.
Wakuu wake walichukua hatua ya kumuonya
polisi huyo baada ya picha yake kusambazwa
kwenye mitandao ya kijamii na kupigiwa gumzo
kubwa.
Alipigwa picha akiwa amevalia sketi yake fupi na
yenye kumbana akiwa anashika doria katika eneo
ambako mashindano ya magari yalikuwa
yanafanyika eneo la Kati mwa Kenya.
Afisaa huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa
kufika mbele ya mkuu wake James Mugeria na
kuonywa vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara
nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni
utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya
heshima kwa polisi
Maafisa mjini Kiambu walisema kuwa kupewa
onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya
kuvalia sketi yake iliyokuwa imembana sana ni
jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa
kuendelea na majukumu yake.
Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa
kuanza kuvalia kiheshima.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti
moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake
kazini mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha
hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya
kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira
kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa
ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya
kumbana. Nini Kauli yako?

#BBC

0 comments:

Post a Comment