Aibu~Hivi Ndivyo Safari ya David Moyes Ilivyokuwa Baada ya Kufukuzwa Man U


Baada ya Moyes kumalizana na Man United na
kuvunja mkataba, hakuna ubishi ilikuwa ni
lazima aondoke na kwenda kupumzika nje ya
England.
Moyes alichagua Marekani, aliona ingekuwa
sehemu nzuri ambayo angeweza kujipumzisha
kabla ya kuanza upya maisha ya mapambano.
Kwa kuwa aliamua kwenda katika Mji wa
Florida akiwa na mkewe na baada ya kulijua
hilo, bilionea Glazer alimpa Moyes ofa nyingine
ya kufikia katika nyumba yake ya kifahari iliyo
mjini humo.
Pia atapata huduma ya usafiri na usimamizi wa
kutembezwa sehemu mbalimbali za jiji hilo na
wasaidizi wa Glazer.
Utaona hivi, kocha akivunja mkataba au klabu
kufanya hivyo. Basi uadui unatangulia na
ikiwezekana viongozi wa klabu hawataki hata
kuzungumza na kocha kwa kuwa anaonekana
kama ni adui.
Glazer ndiye anayepitisha uamuzi wa mwisho,
lakini anaonyesha kiasi gani walivyoachana
kistaarabu na Moyes na hakuna tatizo lolote
lililotokea.
Hivyo mambo yako kitaalamu zaidi ndiyo maana
wakati mashabiki wanaendelea kupiga kelele.
Moyes anakula ‘bata’ Marekani.
Fin.
Moyes amelipwa fedha hizo ambazo
zinajumuisha mshahara wake wa mwezi, fedha
ya kuvunja mkataba pamoja na malipo ya
usumbufu kutokana na uvunjani huo wa
mkataba.
Lakini wakati wa uvunjani mkataba wake, kuna
mambo kadhaa ya kiufundi yalifanyika ambayo
yanaashiria namna gani walioendelea katika
michezo, mikataba yao inavyokuwa na
utaalamu.
Katika mkataba wa Moyes, ilikuwa hivi. Kama
angeifikisha timu katika nne bora na kuweza
kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi
wakimfukuza ilikuwa ni lazima alipwe kitita cha
pauni milioni 9 (zaidi ya Sh bilioni 22.5).
Pamoja na maji kuwafika shingoni, uongozi wa
Man United uliendelea kufanya subira katika
jambo moja. Kuwa iwapo watafungwa mechi
itakayothibitisha kuwa hawatakuwa katika nne,
maana yake wamekosa kushiriki Ligi ya
Mabingwa Ulaya, hapo watatoa pauni milioni 7
badala ya milioni 9.
Mkutano wa mwisho waliofanya wamiliki wa
Man United, Joe Glazer na wenzake ilikuwa ni
kujaribu kuokoa pauni hizo milioni 2 wakati
Moyes anaondoka.
Mechi dhidi ya Everton ndiyo ilikuwa na majibu,
kama Man United wangepoteza maana yake
uhakika wasingefika nne bora na malengo ya
uongozi kuokoa pauni milioni 2 ungekuwa
umetimia.
Baada ya Man United kufungwa mabao 2-0,
viongozi wa Man United waliandaa mkutano
mara moja kumtaarifu kocha huyo kuhusiana na
suala hilo na taarifa zikaanza kuvuja.
Huenda wengi walishangazwa na namna ungozi
wa Man United ulivyochelewa kumuondoa.
Lakini mambo mawili yalikuwa ya msingi zaidi
kwao kuliko matakwa ya mashabiki.
Kwanza kuangalia kama kungekuwa na
mabadiliko ili Moyes aendelee, lakini
kuhakikisha kama imeshindikana, basi na pauni
milioni 2 ambazo si haba, ziokolewe.
Hilo ni moja la kujifunza kwa klabu za hapa
nyumbani namna ambavyo mikataba
inaandaliwa kitaalamu na inakuwa imelenga
mambo kadhaa na hata ukivunjika. Zaidi
unalenda kwenye kufanikiwa na kufeli na si
ilimradi mkataba tu wa kazi, hata wa kocha
unaringana na wafanyakazi wote!
Kitu cha pili cha kujifunza ni

0 comments:

Post a Comment