NAY AFUNGUKIA TUHUMA ZA KUTISHIA KUUA


STAA wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel
Elibariki ‘ Nay wa Mitego ’ amefungukia
skendo ya kumtishia kumuua mdogo wake
aitwaye Amani Shija .
Staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’
Akizungumza na gazeti hili Aprili 29 mwaka
huu, Nay alisema kwamba anasikitishwa
sana na malalamiko ya Amani kwani katika
maisha yake hajawahi kumtishia mtu kumuua
na hajui ni kipi ambacho kimemvuta hadi
kuanza kulalama mambo kama hayo.
“Hakuna ishu kama hiyo , kwanza Amani siyo
ndugu yangu wa damu ila udugu wangu naye
niliutengeneza baada ya kukutana naye
Ubungo miaka minne iliyopita na akaniomba
nimsaidie , bila kinyongo nilianza kuishi naye
hadi leo hii anaanza kunitolea maneno kama
hayo, ” alifafanua Nay na kuongeza :
‘Nay wa Mitego’ akiwa stejini
“Ameshindwa kujielewa lakini mimi
namuachia Mungu maana kama kumsaidia
nimeshamsaidia sana, nshamlipia hadi
chumba zaidi ya miaka minne na
nikamtimizia mahitaji yake yote, lakini wapi .”
Mapema wiki hii , Amani aliripotiwa katika
gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa
amemfungulia mashtaka polisi Nay wa
Mitego kwa madai ametishiwa maisha.

0 comments:

Post a Comment