WOLPER : NATAKA SERIKALI MBILI


MWIGIZAJI staa Bongo, Jacqueline Wolper
ameifungukia rasimu ya katiba mpya ambayo
ipo bungeni kujadiliwa kwa sasa akisema
yeye matakwa yake ni kuwepo kwa serikali
mbili na si tatu wala ya mkataba.
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar , Wolper
alisema anaamini serikali ya tatu itakuwa
mzigo kwa wananchi ambao ndiyo walipa
kodi .
Muigizaji staa Bongo , Jacqueline Wolper
“Serikali mbili ndiyo mpango mzima , ya tatu
ni mzigo, ya mkataba sioni maana yake.
Halafu nataka muungano udumu , pia
nitafurahi sana kama Ukawa watarudi
bungeni litakapoanza tena Agosti mwaka
huu, ” alisema Wolper .

0 comments:

Post a Comment