DENTI AFIA KWA HAWARA


MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa
miaka 20 , mwanafunzi wa Chuo cha Eden
Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha
mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani
kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake,
Hafidh Mohammed .
Mwili wa Atu ukiwa chumbani kwa mtu
anayesadikika kuwa ni mpenzi wake, Hafidh
Mohammed.
Tukio hilo lilitokea April 26 , mwaka huu na
kukusanya umati huku mwanaume aliyelala
na binti huyo akitokomea
kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa
mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.
Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha ,
mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa
eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye
alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi
kulipokucha na kabla ya hapo , hakuwa
akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na msichana huyo kwa vile
aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke
mwingine ambaye alizaa naye .
“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu
ya uhusiano wao na huyu mwanafunzi ,
nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu
huku akionekana kuchanganyikiwa ,
nimejaribu kumsihi asikimbie lakini
imeshindikana,” alisema mama huyo.
Mwili wa Atu ukiingizwa kwenye gari la
polisi .
ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha
masomo ya biashara na habari ambao
walikataa kutaja majina yao waliliambia
gazeti hili kuwa , marehemu Atu aliwaaga
anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza
wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya
Amana, Aprili 23, mwaka huu .
Hata hivyo , walisema uondokaji wake uliwapa
maswali mengi kwani tofauti na
walivyotegemea kuwa angebeba mfuko
mkubwa wenye nguo za kubadili , yeye
aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi
pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali .
Walisema siku tatu baadaye walipatwa na
mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli
yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao
kilichotokea katika chumba cha mvulana
huyo anayeishi jirani .
MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili
walisema kwao haikuwa mara ya kwanza
kumuona msichana huyo, kwani mara kwa
mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia
ndani hakuwa akitoka nje .
Walisema mara zote hizo , mwanaume huyo
mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na
kwenda kumnunulia chakula .
Wananchi na wanausalama wakiwa eneo la
tukio .
POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA
TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na
kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani
ukiwa hauna jeraha , lakini pembeni yake
kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika
ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa
pamoja na mkoba wake hadi kituonis.
Minong ’ ono kutoka kwa majirani kuhusiana
na vidonge hivyo ilitofautiana , baadhi yao
walisema huenda vilitumika katika jaribio la
kutoa mimba , wengine walisema
inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa
wa ghafla usiku na mwanaume huyo
alikwenda kumchukulia vidonge hivyo
ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu
kupata nafuu .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani , SACP
Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kusema juhudi za kumtafuta
mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari
nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini
chanzo cha kifo hicho.

0 comments:

Post a Comment