SIRI YA KUFUKUZA UZEE WA HARAKA


ENZI za uhai wake, marehemu Dk . Remmy
Ongalla aliwahi kuimba hivi : “Nikikumbuka
uzee huwa silali ”. Mungu ailaze roho yake
mahali pema peponi na tutaendelea
kumkumbuka daima . Wakati uzee ni ‘ tunu’ ya
maisha marefu toka kwa muumba, Dk .
Remmy alikuwa halali akiukumbuka tu kwa
kuwa uzee ni msururu wa matatizo mengi
lakini kubwa ni ya kiafya .
Ikumbukwe kuwa kila tukijiangalia
makunyanzi usoni ndiyo tunahisi hali ya uzee
bila kujua hata moyo, mapafu, ubongo , misuli ,
macho n.k . navyo huwa vimechakaa hivyo
kumfanya mzee aishi maisha tegemezi kwa
kila kitu .
Lakini upo uwezekano tena mkubwasana wa
kuufukuza uzee . Uzee hufukuzwa kwa njia ya
vyakula kwa kuchelewesha mchakato wa
mwili kujizeesha .
Ieleweke kuwa mwili wa binadamu ukipata
virutubisho sahihi basi seli za mwili
huboreshwa na mtu hunawiri na kuonekana
kijana hata kama ni mzee . Seli za mwili ndizo
zinazoungana kujenga mwili wa binadamu na
seli hizi zipo hai lakini zinahitaji lishe sahihi
ili ziwe na nguvu inayohitajika .
Seli hizi mara kwa mara hufa na mwili
hutengeneza seli nyingine kufidia zilizokufa
kila baada ya muda fulani. Mwili unaweza
kufidia seli zilizokufa kwa kuzalisha zingine
mpya ambazo zinaweza zikawa ni za aina
moja kati ya hizi tatu :
Ya kwanza ni seli zisizo na nguvu kama
zilizokufa. Seli hufa pale zinapokosa
virutubisho sahihi . Seli zinapokufa hufanya
mwili kuchoka na kuchakaa mapema na
hivyo kumfanya mtu aonekane mzee kuliko
umri wake. Hii kitaalamu huitwa “Body
Degeneration ”.
Aina ya pili ya seli ambazo mwili unaweza
kuzalisha kufidia zilizokufa ni zile ambazo
zitazalishwa nyingine lakini zitalingana ubora
na seli zilizokufa . Aina hii ya uzalishaji seli
huufanya mwili usinawiri na kubaki katika
hali ileile. Upatwapo na maradhi utajikuta
ukirudia dozi kadhaa bila kupona kwa kuwa
mwili huwa umedumaa . Haubomoki wala
haunawiri . Hii kitaalamu huitwa “Chronic
Condition ”.
Aina ya tatu ya seli zinazoweza kuzalishwa
kufidia zilizokufa ni seli zenye ubora na nguvu
kuliko zile zilizokufa. Katika hali hiyo ni
rahisi sana mzee kuonekana kijana kwa kuwa
seli mbovu hufa na huzalishwa seli bora na
imara kushika nafasi ya zilizokufa .
Hii kitaalamu huitwa “Body Regeneration ” na
ndiyo hufukuza uzee ( Anti- ageing Process ) .
Unaweza ukajiridhisha kwa macho tu kama
utafuata taratibu za mlo wenye nguvu za
kuufukuza uzee . Ila, hutakiwi uwe na haraka
ya matokeo wala usitegemee miujiza ya
kuamka na kupata mabadiliko .
Zingatia kila siku ulaji wa vyakula vyenye
asili ya majani na matunda katika kila mlo
wako kwa asilimia 75, huku ukiishinda hulka
ya mdomo kupenda vyakula vitamu visivyo
na tija mwilini .

0 comments:

Post a Comment