WEMA SEPETU AANDIKIWA BARUA NZITO!

KWAKO,
Wema Sepetu , staa wa ukweli unayeng’ ara
kimataifa . Sina wasiwasi nikisema hivyo
maana namaanisha .
Leo nimekukumbuka kwa barua; nimefanya
hivyo mara kadhaa kila ninapokuwa na
jambo la kukushauri .
Kwanza nakupongeza kwa kutwaa taji la
msichana mwenye mvuto wa kimahaba
iliyotolewa na Gazeti la Ijumaa ‘ Ijumaa
Sexiest Girl’ wikiendi iliyopita pale Dar Live,
Mbagala – Zakhem , Dar .
Ushindi wako ni baada ya kuwaacha mastaa
wenzako wengi pembeni hadi kufikia fainali
iliyokukutanisha na Jacqueline Wolper ,
Elizabeth Michael , Jokate Mwegelo na Nelly
Kamwelu.
Vigezo vilizingatiwa lakini kubwa ilikuwa ni
kumsaka msichana mwenye mvuto kuliko
wenzake . Wema , ukijaribu kuangalia safari
yako ya mashindano ya urembo, mara zote
umekuwa ukifanya vizuri. Hujawahi
kuwaangusha mashabiki wako .
Kwanza ulivaa viatu vya Miss Dar Indian
Ocean na baadaye ukawakilisha Kanda ya
Kinondoni kabla ya kupanda Miss Tanzania
mwaka 2006 ambapo uliwabwaga wote na
kuibuka kidedea . Huo ni uwezo wa juu sana.
Nakumbuka katika kipindi kilichokuwa na
ushindani mkubwa ni pamoja na hicho.
Fainali yenu ilikuwa na wasichana wenye
mvuto na sifa hasa, lakini uliweza kupenya na
kufanikiwa kuibuka kidedea . Tangu hapo
umeendelea kuutunza vyema mvuto wako na
hujaonekana kuchuja .
Tangu mwaka 2006 ukiwa na umri wa miaka
18 ( kama ulivyosema ) , leo hii miaka nane
baadaye una miaka 26 na bado unaonekana
katika mwonekano mzuri . Hilo ni jambo zuri
na la kujivunia kwa hakika .
Kwa kuwa shindano lenyewe la Ijumaa
Sexiest Girl lilihusisha wasomaji , bila shaka
walikuchagua kwa sababu wanakukubali
katika mambo mbalimbali ya kijamii
ukiachana na mvuto ambao kilikuwa kigezo
kikuu .
Jambo kubwa kwako ni kuhakikisha
unaendelea kutunza mwonekano wako ,
unashiriki katika mambo mbalimbali ya
kijamii na kufanya vizuri katika kazi yako ya
sanaa ya uigizaji unayoifanya kwa sasa .
Lazima utambue kuwa una jina kubwa na
unakubalika; kazi yako ni kuifanya jamii izidi
kukuamini; wasione walifanya makosa
kukuchagua kwa kura nyingi ili uwe mshindi .
Nakusihi Wema , wewe ni staa , jiweke mbali
na mazingira yanayosababisha skendo . Ishi
kama kijana anayetambua thamani yake .
Wewe ni kioo cha jamii , jitahidi jamii ijiangalie
kupitia kwako.
Ijifunze mambo mengi kupitia wewe . Zile
sarakasi zako , achana nazo ili uendelee
kutunza heshima ya ustaa wako . Habari zako
magazetini acha zitawale , lakini kwa mazuri
tu ! Skendo zikae mbali na wewe .
Ukiamua, inawezekana!
Yuleyule ,
Mkweli daima,
Joseph Shaluwa

0 comments:

Post a Comment