MUME, MKE WATEKWA !


KIJANA aliyetambulika kwa jina la Dickson
Mathias ( 35) , na msichana aliyejulikana kwa
jina la Mariam Kimaya wanadaiwa kutekwa
kwa nyakati tofauti baada ya kufunga ndoa
ya siri katika Kanisa la KKT , Tegeta jijini Dar ,
Mei Mosi, 2012 , Risasi Mchanganyiko
linakupa zaidi .
Mariam Kimaya anayedaiwa kutekwa.
Akizungumza na gazeti hili kwa majonzi
makubwa, dada wa Dickson, Aneth Mbaga
alisema tukio hilo lilitokea baada ya Dickson
kufunga ndoa hiyo na Mariam bila idhini ya
wazazi wake kwenye kanisa hilo.
“Baada ya habari za kufunga ndoa ya siri
kanisani kuwafikia baadhi ya ndugu wa
Mariam, Dickson alianza kupokea simu za
vitisho wakimuuliza ni kwa nini alifunga ndoa
ya siri na binti yao wao wakiwa hawajui ?
“Agosti 10, mwaka jana, nikapata taarifa
kwamba Dickson alitekwa maeneo ya Mbezi
ya Jogoo ( Dar ) na watu wasiojulikana .
Dickson Mathias anayedaiwa kutekwa
pamoja na mkewe.
Walimweleza sababu za kumteka ambazo
mimi sizijui, ” alisema Aneth.
Aneth alizidi kuongeza kuwa miezi minne
mbele , alipata taarifa kuwa , mkewe Mariam
naye alitekwa na watu wasiofahamika, hadi
sasa hajulikani alipo kama vile mumewe.
“Yeyote mwenye taarifa sahihi naomba
aripoti kituo chochote cha polisi kilicho jirani
yake maana ndugu tuna wasiwasi mkubwa,
hata kwa ndugu wa mwanamke nako hakuna
anayejua waliko wawili hao , ” alisema dada
huyo huku akimwaga machozi .
Taarifa za kutekwa kwa Dickson ziliripotiwa
katika Kituo cha Polisi Tabata na kuandikiwa
jalada: TBT /RB/1988 /2013 na polisi bado
wanawasaka wanandoa hao .

0 comments:

Post a Comment