PRODYUZA MANECKY NA MADAI YA KUZAA NA RIYAMA


NYUMA ya mafanikio ya wasanii wa muziki
kuna wengi wanachangia lakini mara nyingi
ni kama hawajulikani .
Prodyuza mkali Bongo kutoka AM Records,
Emmanuel Saimon Sewando ‘ Manecky’.
Hata wakijulikana ,sifa huenda moja kwa moja
kwa msanii tu .Maprodyuza wana mchango
mkubwa sana, maana wakitengeneza ngoma
mbaya, mwisho wake ni kwamba msanii
hawezi kutoka . Leo hapa
kwenye Exclusive Interview tunaye Prodyuza
mkali Bongo kutoka AM Records, Emmanuel
Saimon Sewando ‘ Manecky ’ .
Je , unajua kuwa nyimbo kibao za wasanii
kama Diamond , Suma Lee , Ali Kiba , Keisha na
wengineo zina mkono wake?
Manecky amefafanua mengi juu ya kazi zake
za muziki , maisha binafsi na skendo kadhaa
zinazotajwa dhidi yake.
Msanii wa filamu Riyama Ally
INADAIWA DIAMOND HATAKI KUFANYA
KAZI TENA NA WEWE KWA SABABU
ULIACHIA WIMBO WAKE WA NATAKA
KULEWA BILA RIDHAA YAKE , IMEKAAJE ?
Ujue wasanii wana mchezo ukimaliza kazi
yake, anaomba demo na kuiweka kwenye
simu yake , sasa wana katabia ka kuachia
chinichini ( kwa kuwarushia rafiki zao kwa
simu) ili kusikiliza wadau wanavyopokea .
Ikipokelewa vizuri, anaitoa au akiona ina
upungufu fulani anaifanyia mabadiliko haraka ,
ndicho kilichotokea kwa Diamond .
Mimi nisingeweza kuachia singo yake bila
idhini yake .
Kwanza ili iweje ? Halafu singo yenyewe
iliyoachiwa ilikuwa haina hata lebo yangu ,
sasa ingekuwa na faida gani na mimi ?
Sijambo la kweli .
INAELEZWA UNA UHUSIANO WA KIMAPENZI
NA MSANII WA FILAMU, RIYAMA ALLY NA
UMEZAA NAYE. FAFANUA .
Hapana . Riyama ana maisha yake , ana
mwenzake na mtoto wake.
Kilichopo ni kwamba nipo naye karibu kikazi ,
halafu kwa bahati mbaya, jamaa yake na
Riyama anafanana sana na mimi , nadhani
watu wanashindwa kututofautisha .
LAKINI INASEMEKANA RIYAMA ALIKUPORA
MIKONONI MWA ROSE NDAUKA NA
UHUSIANO WAO SASA SI MZURI , KISA NI
WEWE. UNASEMAJE ?
Siyo kweli . Hata hivyo , sipendi
kumzungumzia Rose kwa sababu ana mtu
wake na kila mtu anajua . Siyo vizuri kusema
chochote
kilichotokea kati yangu na yeye wakati
uliopita .
UNAKUTANA NA CHANGAMOTO GANI
KWENYE ‘GAME ’?
‘ Sometimes’ wasanii hawataki kubadilika ,
unaweza ukamshauri abadilishe baadhi ya
vitu kwenye wimbo wake ili uwe wa tofauti
anakataa. Tatizo wanakariri .
Mfano; nakumbuka wakati natoa idea yangu
kuboresha wimbo wa Hakunaga wa Suma
Lee , hakunielewa. Ilifikia mahali
tukakorofishana studio , lakini mimi nilikuwa
natetea kitu kizuri.
Ona sasa , mwisho wa siku , ngoma imetoka
imekuwa mzuka. Jamaa amepiga shoo nyingi
sana. Ni kwa sababu alitoa kitu cha tofauti .
Sasa hivi wasanii kibao wanamuiga .
TAJA TOP 6 YAKO YA WASANII WA BONGO
FLEVA
Wa kwanza kabisa ni Lady Jaydee , huyu
mdada ni mkali. Ameanza zamani na mpaka
sasa hajachuja . Anajua muziki , amewekeza
kwenye
biashara na anajua anachokifanya .
Wengine ni Ben Pol, Vanessa Mdee, Diamond ,
Ali Kiba na AY. Hawa nawakubali sana. Wapo
kwenye nafasi za juu kwa upande wangu.
KUNA MADAI KUWA WASANII WA KIKE
WANA SHINDWA KUWIKA KWA SABABU
WAKIJA STUDIO MNAWATAKA KIMAPENZI,
IMEKAAJE HIYO ?
( Anacheka sana ) Kama wapo walio
kwamishwa kwa mtindo huo nadhani
wamejitakia wenyewe tu . Hivi msanii kama
amekuja kikazi,
utaweza kujiingiza kwenye mambo ya
kimapenzi ?
Utakuta msanii anakwenda studio , amevaa
kimitego halafu usiku ! Unategemea nini?
Hata sisi ni binadamu bana ( anacheka tena ) .

0 comments:

Post a Comment