MR BLUE: WEMA , NAJMA WALINIFILISI


NYOTA wa Bongo Fleva , Herry Samir maarufu
kama Mr. Blue amesema wasichana
warembo , Wema Sepetu na Najma ambao
aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati
tofauti miaka ya nyuma , walimfilisi kutokana
na matumizi makubwa ya fedha alipotoka
nao viwanja.
Nyota wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu
kama Mr. Blue akiwa kwenye pozi.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni ,
Mr. Blue , msanii aliyeanza kupata umaarufu
akiwa bado kijana mdogo , alisema
alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao ,
kwani vinginevyo wangemuona hana pesa ,
kitu ambacho hakuwa tayari kuona
kinatokea.
“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana
starehe , kila day ( siku ) wanataka twende
kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka
niliyumba kimuziki .
Wema Sepetu a .k. a ' Beautiful Onyinye' .
“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani ,
ila kuna Wema na Najma , ilikuwa ukizama
nao dukani lazima ufanye shopping
( manunuzi ) ya nguvu, kuanzia laki saba,
nane na kuendelea ili wakuone unazo na
mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo,
sms hazikauki kuomba uwatumie mawe
( pesa ) , ” alisema .
Kuhusu maisha yake ya sasa , Mr. Blue
alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa
ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu
na amejaliwa kupata mtoto mmoja , hivyo ni
baba wa familia ambaye pia anakaribia
kumaliza mjengo wake siku si nyingi .
Mrembo Najma.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu , ana
malengo na upendo kwani amekuwa
akimuaga kila safari anayofanya na kwamba
hata yeye anaporejea nyumbani , hupokelewa
vizuri.
Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda
mrefu ambao bado wanafanya muziki na
wenye mashabiki wengi ndani na nje ya
Bongo.

0 comments:

Post a Comment