Wezi kukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'


Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja
wa matajiri wakubwa duniani
Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa
Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za
kiisilamu.
Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni
jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo
itaanza kutumika kuanzia wiki hii.
Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni
pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga
mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya
kushiriki Zinaa.
Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika
kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi
wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za
kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na
Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na
utumiaji wa pombe.
Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha
Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah
na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje
mafuta na gesi yake.
Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika
nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza
ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo
akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha
wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria
hiyo.
Sheria yenyewe itaanza kutumika katika kipindi
cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya
kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa
faini.
Katika awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza
kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia
ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa
mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja.
Sultani anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa
matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya
watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia
mitandao ya kijamii.
Mfumo wa sheria katika mahakama nchini humo
ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha
mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo
inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki
za binadamu.

Source: BBC

0 comments:

Post a Comment