JOKATE, NATURE WATIFUANA!


PASUA jipu! Mastaa wawili wenye majina
makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate
Mwegelo ‘ Kidoti ’ na Mbongo- Fleva Juma
Kasim ‘ Juma Nature ’ wanadaiwa kuacha
mshangao kwa wasanii wenzao baada ya
kutifuana, Ijumaa Wikienda limeng’ atwa sikio .
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘ Juma
Nature ’.
Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga
kutomaindi lakini habari za kushangaza
zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke
amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo
kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya
ndala au kandambili .
Kabla ya madai haya mapya , Nature aliwahi
kunukuliwa redioni wakati akitambulisha
wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa
yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni .
Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature
amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘ amekopi’
na ‘ kupesti’ wazo lake la biashara .
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti ’.
Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa
akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa
bila mafanikio .
“Nature amekuwa akimpigia simu Jokate
lakini haipokelewi, ” kilidai chanzo hicho kwa
sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu
wa bastola .
Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika
kuziona kandambili za Jokate lakini
amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa
mrembo huyo kamuibia .
NATURE AFUNGUKA
Alifunguka : “Hadi sasa hivi sijabahatika
kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu
wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo
langu.
“Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao
sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu
mbaya.
“Kweli sikutegemea kama ishu kama hiyo
ingefanywa na mtu kama yeye ( Jokate ) ila
hata kama ametoa mimi wazo langu liko
palepale .“Nitakuja kuzitoa tu hizo kandambili
zenye picha na jina langu. ”
Kandambili zilizosababisha mtifuano .
BOFYA HAPA KUMSIKIA JOKATE
Baada ya kusikia upande mmoja wa Juma
Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa
habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na
kumsomea mashitaka yake hayo ya kuiba
wazo la biashara la Juma Nature .
Bila kupepesa macho wala kuchezesha
masikio , Jokate alifunguka kwamba kwa
upande wake anasikitishwa na mtu kama
Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu
anaowaheshimu.
Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza
kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake .
“Wewe siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo
kutoka kwa Nature , niliamini baada ya mimi
kutoa hizo ndala , atanisapoti kwani mimi
niko katika kuendeleza na kutoa ajira kwa
vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu
letu la maisha .
MASIKITIKO
“Kweli Nature amenisikitisha sana kwa
kitendo chake cha kunitangazia ubaya.
“Hata hivyo , siwezi nikaacha kutoa bidhaa
zangu, nitaendelea kutoa ‘ so ’ itabidi tu
anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za
kwake,” alisema Jokate, mmiliki wa lebo ya
mavazi ya Kidoti.
MASTAA WANASEMAJE KUHUSU SAKATA
HILO ?
Wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya
mastaa ambao walionesha kushangazwa na
sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na
Nature kuhitilafiana wakati kazi zao
zinategemeana .
“Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo
tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni
watu ambao muda wowote wanaweza
kukutana kwa ajili ya kufanya kazi , ” alisema
mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Bongo
Fleva .
NATURE KAMGEUKA JOKATE ?
Kwa mujibu wa mastaa hao, awali Nature
aliposikia Jokate ana ‘ aidia ’ kama hiyo
alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii
mwenzake hivyo kipato atakachopata
kitamsaidia maishani lakini kumbe
inawezekana kimoyomoyo ilimuuma ndiyo
maana ameendelea kumtuhumu Jokate.
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Ni vyema Jokate na Nature wakakaa na
kukubaliana waifanye biashara hiyo kwa
pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa
zaidi , ni kiasi cha kuona fursa na kuitumia .

0 comments:

Post a Comment