SOMO SAHIHI LA KUPUNGUZA MAWAZO NA KUONGEZA FURAHA!


MUELEZE HUJISIKII VIZURI
Ikibidi sema unaumwa . Mpenzi bora
atapunguza maswali au baadhi ya vitu na
kukuacha upumzike . Hiyo itakusaidia
kuingiza hewa kichwani ambayo
itakuongezea nafasi na mwisho kichwa
kitakuwa chepesi.
Maneno ya hapa na pale ukiwa na msongo
wa vitu kichwani , utaona kama ni vuvuzela
zinapulizwa masikioni . Unapomuomba
mwenzio akupe nafasi ya kupumzika kwa
sababu hujisikii vizuri, itakusaidia kupunguza
uzito wa kichwa .
ANGALIZO ;
Unapaswa kuwahi kujieleza kabla mwenzako
hajaanza yake, kwa maana akisema yeye
halafu wewe ndiye ufuate, atajua umeamua
kumkwepa .
LALA USINGIZI
Tafuta usingizi kisha utokomee kwenye njozi ,
ukiamka hutokuwa yule yule . Angalau kichwa
kitakuwa kimepumua na uzito umepungua.
MUELEZE KINACHOKUSUMBUA
Ni tiba kwako endapo utafungua kinywa na
kumueleza mwenzio kile ambacho
kinakusumbua. Atajua kinachokusibu , kwa
hiyo atajua jinsi ya kukuzoea kuliko kufika na
kukaa kimya au kumjibu mkato au kufoka bila
mpango.
CHAGUA KINACHOKUFURAHISHA, FANYA
Unapenda kungalia filamu au kingine
chochote na unaamini ukikifanya
kitakuondolea hasira , basi fanya ili kujiweka
vizuri kisaikolojia mbele ya mwenzi wako .
Kuna wale ambao hasira zao hutoweka
baada ya kupanda kitandani , nalo si tatizo
ilimradi kutibu hasira .
Angalizo ni kwamba kupanda kitandani
kunahitaji uhuru wa hisia . Utazungumza vipi
na mwenzi wako mpaka mkubaliane kupeana
hiyo dawa? Muhimu ni kumueleza
kinachokusibu , akikuhurumia, basi huo ndiyo
uwe mwanzo wa kutii kiu .
UVUMILIVU
Yote ni muhimu lakini uvumilivu ni kitu cha
msingi. Jifunze kusikiliza vitu bila kutoa
majibu. Acha baadhi ya mambo yawe fahari
ya masikio . Inawezekana umesikia na jibu
unalo lakini unatakiwa uitambue hali
uliyonayo , kwa hiyo endelea kunyamaza .
Ukiweza hili basi umefaulu mtihani mgumu
na haitatokea ugombane na mwenzio kisa
umeudhiwa kazini kwako au kwenye
daladala.
HITIMISHO
Zingatia hayo ambayo nimekudokezea
mwanzo mpaka mwisho . Hivyo ndivyo
unavyoweza kuongeza furaha yako na
kupunguza mawazo. Nakusisitiza kupiga vita
msongo wa mawazo kwa sababu mara nyingi
hupoteza njia. Mhusika hukosa mwanga wa
kupata ufumbuzi .
Unapokosa ufumbuzi , itakusababishia
kufanya uamuzi ambao siyo sahihi , hivyo
kukuelekeza kwenye majuto ya baadaye.
Hakuna sababu ya kujuta , shughulikia
mambo yako kwa utaratibu . Makala haya ni
dira yako katika kukupunguzia mawazo na
kukuongezea furaha.

0 comments:

Post a Comment