DENTI MIAKA 12 AOLEWA


YELEUWII! Kuishi kwingi ni kuona mengi,
kijana aliyejitambulisha kwa jina la Andrew
Vincent ( 23 ) ambaye amemaliza kidato cha
nne mwaka jana , amejikuta katikati ya
matatizo kufuatia kufunga pingu za maisha
na mwanafunzi wa darasa la tano
aliyefahamika kwa jina moja la Wastara ( 12) ,
wote wakazi wa Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wastara akifanya usafi ndani kwake baada
ya kuolewa .
Tukio hilo lilijiri Aprili 26 , mwaka huu ambapo
kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu
‘ OFM ’ kilipokea taarifa kutoka kwa
wasamaria wema wakilalamikia kitendo hicho
na kutaka mwanafunzi huyo asaidiwe ili arudi
shule .
OFM kama kawaida yake , ilitinga eneo hilo
kwa ajili ya kufuatilia taarifa hizo ambapo
iliweza kuungana na mwalimu mkuu wa
shule ya msingi anayosoma ‘ bi harusi ’ huyo ,
Hamad Mnaguzi na viongozi wengine wa
kamati ya shule akiwemo mwenyekiti wa
serikali ya kijiji, Shaban Zageni .
Kijana aliyefahamika kwa jina la Andrew
Vincent anayetuhumiwa kuoa mwanafunzi .
OFM na viongozi hao walikwenda nyumbani
kwa wazazi wa mtoto aliyeozeshwa na
kumkuta mama yake aliyejitambulisha kwa
jina la mama Wastara huku akikataa kutaja
alikokwenda baba wa mtoto huyo pamoja na
wanandoa wenyewe.
OFM ilipomuhoji kama anatambua tukio la
mtoto wake kuozeshwa alikataa kuwa , hana
mtoto wa shule ambaye ameolewa hivi
karibuni huku akidai kuwa yeye ana mtoto
mmoja tu ambaye aliolewa miaka mitatu
iliyopita.
Baada ya kubanwa, ndipo akakiri kumuozesha
bintiye na kudai kuwa familia ilifanya hivyo
kutokana na ugumu wa maisha .
Hata hivyo , mama huyo akasema hajui
makazi ya mwanaume huyo yalipo .
OFM kwa kushirikiana na viongozi hao wa
serikali walimchukua mama huyo hadi
kwenye ofisi ya serikali ya mtaa huo na
kumlazimisha aelekeze alipo mwanae ndipo
mjomba wa Wastara alijitokeza na kusema
anapajua walipo wanandoa hao .
Saa 3 usiku , OFM na viongozi hao walifika
kwenye kituo cha mafuta kilichopo Msata,
Bagamoyo, Pwani na katika uliziaulizia,
nyumba hiyo ilipatikana ambapo bwana
harusi na baba yake walikimbia .
OFM ilifanya jitihada za kumsaka kijana huyo
na kufanikiwa kumnasa na kumhoji kwa kina
sababu ya kuoa denti wa shule ya msingi
ambaye walimu wake wanamtambua kuwa ni
mwanafunzi wao , akajitetea kuwa ,
aliwasiliana na wazazi wa binti huyo baada
ya kukutana naye njiani na kuvutiwa kumuoa .
Wastara akiwa na begi lake .
“Mimi sikujua kama mwanafunzi niliambiwa
hasomi, najuta! Hapo nimetoa mahari shilingi
300, 000 lakini sina budi kuachana naye , ”
alisema kijana huyo.
Akaendelea : “Nimelala naye siku moja tu
baada ya ndoa , ni vyema wanirudishie mahari
yangu.”
Kwa upande wake denti huyo alisema
hakuwa tayari kuolewa mapema ila kwa
kuwa alikuwa haendi shule akaona bora
afanye hivyo .
Baada ya mahojiano hayo, OFM na viongozi
hao walimwamuru binti arudi kwa wazazi
wake ili kufanyiwa mpango wa kuendelea na
masomo huku wanandoa hao wakiangua vilio
kwa kuwa ndoa yao ilikuwa bado changa.

0 comments:

Post a Comment