WASANII WAMFANYIA VIBAYA MTITU MSIBANI


Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo
wameshindwa kuonesha utu ipasavyo kwa
msanii mwenzao , William Mtitu ambaye hivi
karibuni alifiwa na baba yake mzazi .
Baba wa msanii huyo, John Mtitu alifariki
dunia baada ya kusumbuliwa na uvimbe
kichwani na alipofanyiwa upasuaji, hakuweza
kuzinduka .
Wasanii mbalimbali wakiomboleza msiba wa
babaake Mtitu
Siku ya kuaga mwili
Katika hali ya kushangaza, wasanii waliofika
nyumbani kwa msanii huyo, Mburahati jijini
Dar walionesha kususia baadhi ya vitu na
kuwafanya waombolezaji kuwashangaa.
Wasusia chakula
Licha ya mara kadhaa wasanii hao kutakiwa
kwenda kuchukua chakula , wengi
walionekana kujifanya kama hawasikii huku
wakiendelea kupiga stori zao.
Cha kushangaza zaidi , baada ya msosi
kuisha , baadhi walienda kuagiza soda na keki
kitendo kilichotafsiriwa kuwa , walikuwa na
njaa lakini walifanya makusudi kususia
chakula .
Kanisani nako
Baada ya zoezi la chakula , mwili uliingizwa
nyumbani kwa dakika tano na baadaye
ukapelekwa katika Kanisani la Katoliki
Parokia ya Mburahati kwa ajili ya ibada kabla
kusafirishwa kwenda Njombe , Wilaya ya
Ludewa kwa ajili ya mazishi lakini cha
kushangaza nako wasanii hao waliishia nje .
Wakiandaa jeneza kwa ajili ya mazishi
Kuzika sasa
Baada ya ibada kanisani , tangazo lilitolewa
kwamba daftari litapita kwa ajili ya watu
wanaotaka kusafiri kwenda kuzika lakini cha
kuhuzunisha katika hilo pia walikausha ila
akajitokeza mwanadada Sabrina Rupia ‘ Cath ’
kwenda kumfuta machozi Mtitu .
Hatua hiyo iliwafanya wengi waone kuna
tatizo kwa wasanii hao hasa wa Bongo Muvi
kwani haikuwa sahihi kumuacha mwenzao
ambaye pia ni kiongozi wa kundi hilo kwenda
kumzika baba yake bila kampani .
Ikizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Bongo
Muvi, Steven Mengere ‘ Steve Nyerere ’
alisema : “Tulitoa ushirikiano katika kila
jambo , huwezi kumlazimisha mtu kula wala
kuingia kanisani . Kama kuna walionunua
soda na maandazi kisha kula pale ,
wamekosea sana. Chakula kilikuwepo cha
kutosha , kwa nini wafanye hivyo ?”

0 comments:

Post a Comment