Wiki hii
mitandao ya
Nigeria
iliripoti kuwa
kulikuwa na
ugomvi
mkubwa kati
ya mapacha
wanaounda
kundi la
PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba
walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.
Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka
yao mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude
Okoye iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa
huenda ameachana na kundi hilo baada ya
kuwepo ugomvi kati yake na ndugu hao
kutokana na msimamo wake wa
kutohudhuria ndoa ya kisasa ya mdogo wake
itakayofanyika Dubai.
Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye
hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola
Omotayo.
“After over 10 years of hard work, it’s over.
Am done.” Alitweet Jude Okoye.
Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo
anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha
habari hizo wakati akiongea na Premium
Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo
zimetoka wapi.
“I am too busy to give some wanna be
blogger traffic, I don’t know where that
report is coming from. Maybe they just want
to get traffic to their site. It’s baseless and
untrue.” Amesema Bayo Adetu.
ZILE TETESI ZA KUVUNJIKA KWA KUNDI LA P-SQUARE HUU NDIO UKWELI SOMA HAPA
1:38 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment