Karibu robo ya watu wote wanaosafiri wakiwa
wamejificha katika gurudumu la ndege hufariki
Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 16
amenusurika kifo kwa maajabu baada ya
kujificha na kusafiri katika gurudumu la ndege
iliyokuwa ikielekea mjini Carlifornia kutoka
Hawaii nchini Marekani.
Safari hiyo ilidumu kwa saa 5.
Hali yake inadaiwa kuwa shwari licha ya vipimo
vya juu vya baridi baada ya ndege hiyo kusafiri
juu ya bahari ya Pacifiki kwa saa tano.
Msemaji wa shirika la ndege la Hawaii, alisema
kuwa wafanyakazi wa shirika hilo walimuona
kijana huyo baada ya ndege kutua Jumapili
asubuhi.
Alihojiwa na FBI na kupewa huduma ya dharura
huku wauguzi wakisema afya yake iko shwari.
Mvulana huyo anasemekana kutoroka nyumbani
na kuruka ukuta katika uwanja wa San Jose ili
kuweza kusafiri kwa ndege hiyo.
''Wasiwasi wetu mkubwa ni hali hali yake ya
kiafya, alibahatika sana kuwa hai baada ya
kusafiri chini ya gurudumu la ndege kwa saa
tano,'' alisema masemaji wa shirika hilo la ndege.
"huyu mtoto ana bahati sana kuwa hai,''
aliongeza kusema msemaji wa shirika la FBI.
Inaarifiwa punde tu baada ya ndege kutua, kijana
huyo alishuka na kuanza kurandaranda katika
uwanja wa ndege.
Kijana huyo alipatikana tu akiwa na kichana
mkononi.
Aliponea sana, maana alikosa hewa huku
akipigwa na baridi kali ndege ilipokuwa inaruka
mita 12,000 juu angani.
Kadhalika kijana huyo anaarifiwa kupoteza
fahamu muda wote wa safari.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment