BOOOM! Katika hali ya kushangaza, mastaa
wawili Bongo, mwigizaji Wema Isaac Sepetu
na mtangazaji wa DTV , Penniel Mungilwa
‘ Penny’ wanadaiwa kuipasua familia ya
kinara wa Bongo Fleva , Nasib Abdul
‘ Diamond Platnumz ’ , Ijumaa Wikienda lina
ripoti kamili .
Wema akiwa na Diamond Platinum .
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni
mtu wa karibu na familia hiyo kuna
mgawanyiko ambao umesababisha mpasuko
unaofanya familia hiyo kuwa na makundi
mawili yasiyoelewana juu ya uhusiano wa
Diamond na warembo hao .
Penny kushoto katika Pozi tofauti tofauti na
mashosti zake .
Kwa sasa Diamond anatoka kimapenzi na
Wema baada ya kumwagana na Penny lakini
mtangazaji huyo anadaiwa kuendelea kwenda
katika familia hiyo kwani asilimia kubwa
inaonesha anakubalika zaidi ya wengine
wote.
Mtangazaji wa DTV , Penniel Mungilwa
‘ Penny ’ akipozi .
TEAM PENNY VS TEAM WEMA
Habari zilidai kuwa mpasuko huo ni mkubwa
kwani kundi moja linalojiita Team Penny
linamkubali zaidi Penny na lingine ambalo
lina watu wachache Team Wema linamkubali
Wema . Imefahamika kwamba kundi
linalomkubali Penny na kumuona ndiye
mwanamke sahihi kuwa na Diamond
japokuwa wameshaachana ni Mama Diamond
mwenyewe , Sanura Kassim ‘ Sandra ’ , dada
zake Esma Platnumz, Queen Darleen, Anko na
dada wa hiyari wa Diamond , Halima Haroun
‘ Kimwana ’ .
Wema akiwa na Rommy Jones .
Ilidaiwa kwamba kundi hilo limekuwa likitoa
ushirikiano wa karibu mno kwa Penny na
sehemu nyingi wanakuwa wote ikiwemo
kwenye sherehe na viwanja vya starehe ,
yaani ni fulu kujiachia .
Habari hizo zilidadavua kuwa hata dada wa
Diamond , Esma anaishi nyumba moja na wifi
yake huyo wa zamani.
Mama Diamond Sanura Kassim ‘Sandra ’
akiwa na Penny .
“Familia ya Diamond imegawanyika katika
makundi mawili , kundi kubwa linamkubali
sana Penny japokuwa alishaachana na
Diamond . Ilisemekana kuwa si familia tu
kwani hata madansa wa Diamond
wanampenda sana Penny kuliko Wema ,”
kilisema chanzo.
Baba Diamond, Abdul Jumaa .
TEAM WEMA HII HAPA
Uchunguzi wa wanahabari wetu ulibaini kuwa
ndani ya kundi linalomtaka Wema kuna watu
wachache akiwemo Diamond mwenyewe ,
baba yake, Abdul Jumaa ambaye kwa upande
wake alitamka wazi : “Wema ndiye mkwe wa
ukweli kabisa . ”
Baba huyo alikwenda mbali na kusema
anamkubali Wema kwa sababu ana nyota
kali na ana roho nzuri hivyo akiendelea kuwa
na mwanaye atakuwa na mafanikio tofauti na
alivyokuwa na Penny.
Pia ilijulikana kuwa kundi hilo lina mtu
mwingine , ndugu wa Diamond aitwaye
Rommy Jones ambaye amekuwa akionekana
na Wema mara kwa mara hasa wakati msanii
huyo akiwa amesafiri .
HALIMA KIMWANA AITWA KIGEUGEU
Taarifa nyingine zilidai kwamba katika sakata
hilo, Halima kimwana amekuwa akiitwa
kigeugeu kutokana na kutokuwa na upande
anaosimamia. “Mara utamuona na Wema
ghafla unamuona tena na Penny, yule hata
haeleweki . Anajichetua sana, ” kilisema
chanzo chetu .
MAMA DIAMOND ANASEMAJE?
“Mimi siwezi kumchagulia Diamond
mwanamke wa kuwa naye , yeye mwenyewe
ataamua kwa sababu ni mtu mzima kwa hiyo
siwezi kumpangia au kumchagulia
mwanamke wa kuwa naye ,” alisema mama
Diamond bila kukanusha kuwa na ukaribu
zaidi na Penny.
MSIKIE HALIMA KIMWANA
Baada ya kuwatafuta Diamond , Wema na
Penny bila mafanikio , Ijumaa Wikienda
lilizungumza na Halima Kimwana ambaye
alikuwa na haya ya kusema :
“Sisi tuko karibu na Penny kwa sababu
anapenda kujichanganya na sisi hivyo hata
Wema akija kutuchukua na kutaka twende
naye klabu hatukatai kwa sababu wote ni
mawifi zetu .
“Hatubagui kwani hakuna siku ambayo Wema
alishataka kuwa na sisi tukamkatalia .”
MASWALI
Hivi karibuni picha za Penny akiwa na mawifi
zake kwenye shughuli ya kumtoa mtoto wa
ndugu yao zilivuja ambapo ndani ya sherehe
hiyo pia Diamond alikuwepo akiwa anacheza
dufu lakini Wema hakuonekana, jambo
lililozua maswali .
WEMA PENNY WAIPASUA FAMILIA YA DAIMOND
7:41 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment