KAMA kuna kitu kinakukwaza ndani ya moyo
wako , siku zote ukikaa nacho kitazidi
kukuumiza lakini ukiamua kumtafuta mtu
ambaye umeshibana naye na kumsimulia,
moja kwa moja utakuwa umeutua mzigo !
Wema Isaac Sepetu ‘Madam ’ akiwa Kajala
Masanja .
Hicho ndicho amekifanya Miss Tanzania
2006/07 , Wema Isaac Sepetu ‘ Madam’ kwa
kuweka kweupe chanzo cha ugomvi wake na
staa mwenzake, Kajala Masanja huku akijuta
kumlipia mwanadada huyo zile Sh . milioni 13
za faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza na Ijumaa katika exclusive
interview Jumanne iliyopita, Wema ambaye
pia ni staa mkubwa wa sinema za
Kibongoalisema kuwa kuna mambo mazito
ambayo yamesababisha yeye kuingia kwenye
gogoro kubwa na Kajala .Wema au Beautiful
Onyinye alisema kwamba mambo hayo ndiyo
yamemsababishia maumivu ya moyo na
kutokwa machozi kila wakati.
“Leo ( anataja jina la mwandishi) , ngoja
nikuelezee kila kitu kinachohusiana na mimi
na Kajala juu ya tofauti zetu. “Naamini baada
ya kusimulia kisa na mkasa nitakuwa
nimeutua huu mzigo mkubwa nilionao ndani
ya moyo wangu .
“Baada ya hapo sitapenda tena kuzungumzia
ishu inayonihusu mimi na Kajala , ” alianza
kufunguka Wema .
UZINDUZI WA KIGODORO
Katika maelezo yake, cha kwanza , Wema ni
uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro uliofanyika
hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Dar Live,
Mbagala - Zakhem jijini Dar ambapo yeye
alisema kuwa alianza kuyaamini yale
yaliyokuwa yakisemwa na watu kuhusiana na
Kajala .
Wema alisema kabla ya tukio , akiwa saluni
akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi huo , ghafla
Kajala alimharibia ‘ mudi ’ . “Unajua ile Saluni
ya ( anataja jina la saluni ) pale Kinondoni, ina
sehemu mbili , juu na chini , sasa mimi
nilikuwa juu na Aunt ( Ezekiel ) tunatengeneza
nywele .
“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele ,
nikamuona Kajala , kwa kuwa nilikuwa
sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno
yalishaanza kuwa mimi na Kajala tuna bifu ,
nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye .
“Kweli nilipiga makelele ya furaha
nilivyomuona K , nikawa nakimbia kwenda
kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu
baada ya kunikwepa na kusema
nooo. .. Wema usinikumbatie na kuanza kutoa
maneno ya dharau eti nitamchafua .
“Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona
kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa
ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi ,
basi huwezi kuamini , nilishindwa kujizuia
nikajikuta namtukana , sikumbakisha .
“Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye
kiti cha kuoshwa , nikaenda nikamsukuma na
kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe ,
huwezi amini hali ya hewa iliharibika ghafla
kwani sikuwa na mudi tena ,” alitiririka Wema .
SAFARI YA ARUSHA KATIKA SHOO YA
MIRROW
Wema alisema kuwa baada ya kutofautiana
pale saluni , hakuwa na kinyongo, safari ya
Arusha ilipofika walikwenda kumsapoti msanii
wao wa Bongo Fleva anayesimamiwa na
Kampuni ya Endles Fame Production.
Wakiwa njiani, kwa mujibu wa Wema , yeye
alikuwa hana fedha taslimu za kutosha zaidi
ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti
hivyo alimwambia Kajala ampe shilingi laki
tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani
pamoja na matumizi madogomadogo.
Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu
akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.
Aliendelea kutoa ya moyoni: “Tulipofika
Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja
anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue
fedha alizokuwa nazo akamuwekee benki kwa
sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa
eti nilijishaua kuandaa shoo nikitegemea
fedha zake.
“Wakati K anazungumza hivyo kulikuwa na
watu watatu, mimi sina hili wala lile
nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni ,
wamekwenda wapi ?
“Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia
kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu
themanini, kiukweli iliniuma sana,
Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa bali
alinikopesha ?
“Nilijiuliza amesahau mimi nilitoa Sh . milioni
13 kumlipia faini asiende jela miaka saba?
Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare,
viatu sare, mapochi sare, ninachokula na
kunywa mimi ndicho hichohicho.
“Siku zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu,
hereni yaani kila kitu nilikuwa ni mimi, leo
laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima
ananitangazia kwa watu ( anataja jina la
mwandishi)?
“Iliniuma sana basi palepale , nikaenda benki
nikatoa Sh . milioni mbili, nikamlipa fedha
zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote
kinachoendelea kwani ningefanya chochote
ningeharibu shoo na isingekuwa na maana
yoyote ya sisi kwenda Arusha. ”
WAREJEA DAR , MAANDALIZI YA FILAMU
YAKE YAANZA
Wema alisema waliporejea Dar , alimwambia
Kajala kuwa kuna mtu aliyekuwa amempa
stori hivyo alimuomba wafanye filamu wawili.
Alisema kwamba Kajala alikubali na kusema
kuwa atachangia Sh . milioni tano katika
bajeti ya filamu hiyo . Baada ya kusikia hivyo ,
Wema alisema alifarijika, alipokwenda
kumweleza ‘ bebi ’ wake, Nasibu Abdul
‘ Diamond Platnumz ’ , naye Diamond akasema
atatoa Sh . milioni tano hivyo jumla itakuwa
Sh . milioni kumi ikapita bajeti iliyokuwa
imepangwa ya Sh . milioni nane.
Anaendelea: “Tukiwa katika maandalizi ya
mwisho tuanze ku - shoot , K alinipigia simu
akaniambia hawezi ku - shoot kwani alikuwa
na safari ya kwenda China labda wa -shoot
vipande vyake , nikamwambia basi aende
akirudi tutatengeneza nyingine .
“Baada ya kuona hivyo ndipo nikamchukua
Aunt tutengeneze filamu . K alipoona
nimemchukua Aunt, akanipigia simu na
kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza mbona
mwenzangu amesahau ghafla wema wangu
niliomtendea au kwa kuwa tangu aanze
vijisafari vyake vya kwenda China anapata
WEMA : NAJUTA KUMLIPIA KAJALA MIL 13!
12:37 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment