AUNTY LULU ACHEZEA KICHAPO


MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo
‘ Aunty Lulu’ hivi karibuni alijikuta akichezea
kichapo kutoka kwa mpenzi wake
anayejulikana kwa jina la Amani baada ya
kutaka kwenda klabu usiku bila kumtaarifu.
Msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo
‘Aunty Lulu ’ akipozi .
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo lilitokea
mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
walimsikia msanii huyo akipiga mayowe na
walipotoka walimuona akipigwa .
“Kwa kweli alipigwa sana na sasa amevimba
uso,” alidai mmoja wa majirani aliyeomba
hifadhi ya jina lake .
Paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu lakini
hawakuweza kuonana naye kwani aligoma
akidai kwa hali aliyonayo hawezi kuonana na
waandishi ila akasema:
“Ni kweli Amani kanipiga , kaniumiza ila
siwezi kuliongelea sana suala hilo, haya ni
mambo yetu binafsi. ”

0 comments:

Post a Comment