MFANYABIASHARA maarufu wa simu za
mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar ,
aliyefahamika kwa jina moja la Devi , hivi
karibuni alipatwa na soni ya aina yake baada
ya kukutwa katika nyumba ya kulala wageni
akiwa na mke wa rafiki yake wa karibu .
Mfanyabiashara maarufu wa simu za
mikononi maeneo ya Kariakoo jijini Dar ,
anayefahamika kwa jina moja la Devi baada
ya kufumaniwa na mke wa rafikiye.
Mtoa habari makini aliliambia gazeti hili kuwa
kisa kizima kilianza baada ya mwenye mali
( mume ) kukuta ujumbe mfupi wa simu katika
kilongalonga cha mkewe unaoashiria mambo
ya mapenzi na mbaya zaidi , meseji hiyo
ilitoka kwa rafiki yake huyo.
Licha ya kukuta ujumbe huo wa kimahaba ,
chanzo chetu kilidai kuwa pia mume huyo
alikutana na sms kadhaa zilizokuwa
zimetuma fedha kwa njia ya mtandao wa
simu, zikielekezwa kwa dada huyo kwa ajili
ya matumizi yake .
Wafumaniwa hao wakiwa chini ya ulinzi wa
makamanda wa OFM .
Baada ya jamaa huyo kujiridhisha kuwa Davi
alikuwa na nia mbaya na mkewe , mume huyo
aliamua kuanzisha mkakati na kumtuma
mdogo wake kufuatilia ishu nzima kwani yeye
alibanwa na majukumu mengine ya kikazi.
Bila kujua kuwa nyendo zao zinafuatiliwa ,
Davi na shemeji yake walipanga kukutana
katika hoteli moja ( jina linahifadhiwa) iliyopo
Sinza na baada ya kupata chumba na kuingia
ndani, bila hofu , walianza kujiandaa kwa ajili
usaliti.
Mke wa mtu baada ya fumanizi hilo .
Huku mwanaume akiwa ameshatoa nguo
zake sambamba na mpenzi wake , mlango wa
chumba chao uligongwa, lakini wakiwa
hawana hofu , wakiamini ni mhudumu
walifungua na wote kupatwa na bumbuazi
baada ya kugundua aliyekuwa mbele yao ni
mdogo wa mwenye mke ambaye wote
wanamfahamu!
“Huwezi kuamini, baada ya sisi kuingia
chumbani na kuwakuta kama walivyozaliwa,
jamaa alikimbilia chooni na kwa jinsi
alivyokuwa, alionyesha kabisa kuhitaji
kujitumbukiza, lakini bahati nzuri vyoo vile ni
vya kisasa ,” kilidai chanzo hicho.
Mwandishi wetu alimtafuta kwa njia ya simu
mwenye mke kutaka kujua kilichoendelea
baada ya tukio hilo ambapo alipopatikana
alisema :
“Ni kweli tukio hilo limetokea ila siwezi
kuzungumzia zaidi , jamaa alikuwa
akinizunguka kwa mke wangu lakini arobaini
yake imefika, zaidi nenda Kituo cha Polisi
Oysterbay utaelezwa kila kitu. ”
MFANYABIASHARA KARIAKOO AKUTWA GESTI NA SHEMEJIYE GESTI
12:50 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment