Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania
imezindua mpango wa kutoa bure huduma za
mtandao wa kijamii wa Facebook kwa lugha ya
Kiswahili.
Huduma hiyo inayotolewa kwa mara ya kwanza,
itawanufaisha wateja wake wote nchini na wale
wa nchini nyingine za Afrika Mashariki.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa ushirikiano
huo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa
Tigo, Diego Gutierrez alisema ushirikiano huo
utawawezesha wateja wanaotumia mtandao wa
Tigo kuperuzi kwenye Facebook kupitia simu zao
za mkononi bila gharama zozote na kwa lugha
ya Kiswahili badala ya Kiingereza.
“Ni fursa ya pekee itakayowawezesha watumiaji
wetu wapatao milioni mbili kuungana na wenzao
wanaotumia mtandao huo wa kijamii ndani na
nje ya nchi bila kikomo,” alisema Gutierrez na
kuongeza:
“Hii ni mara ya kwanza kwa mtandao wowote
mkubwa wa kijamii kupatikana kwa lugha ya
Kiswahili… lugha ambayo inatumika kwa
Watanzania na watu wa Kanda ya Mashariki na
Kusini mwa Afrika.”
Mkurugenzi huyo alisema mtandao wa kijamii
wa Facebook umekuwa chachu kubwa ya
utumiaji wa data na kwa kulitambua hilo,
wameamua kuwaletea wateja wao ladha mpya
ya kutumia mtandao huo kwa lugha yao asilia ili
kunufaika zaidi kulioko kutumia mtandao kwa
lugha ya kigeni.
“Hii ndiyo maana halisi ya maisha ya kidigitali
(digiti)… huduma hii mpya itafungua milango
mipya ya kielimu, biashara na kiuchumi kwa
watumiaji wa mtandao wetu duniani.”
Tanzania ni nchi ya pili kupata fursa ya
kuzinduliwa kwa huduma hiyo. Paraguay ilikuwa
ya kwanza kupata huduma sawia na hiyo
ambayo ilizinduliwa Desemba mwaka jana na
watuamiaji wa mtandao wa Tigo walianza
kutumia huduma hiyo kwa lugha yao ya
Kiguarani.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Facebook wa
Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Nicola D’Elia
alisema ushirikiano huo ni wa kwanza nchini
kwa kushirikiana na kampuni hiyo ya simu
kuwapatia Watanzania wengi uwezo wa
kuwasiliana kwa lugha yao na kupata huduma za
data bure.
TIGO KUTOA HUDUMA YA FACEBOOK KWA KISWAHILI
3:09 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment