NYUMBA ALIYOIJENGA LULU YATUMIKA KWA KUTAPELI


Mjengo wa staa wa filamu za Bongo,
Elizabeth Michael ‘ Lulu’ uliopo Mbezi
Temboni - Salanga jijini Dar es Salaam
umeingia kwenye lawama kufuatia madai
kwamba, unatumika kwa kutapeli watu
wanaotaka kununua nyumba maeneo hayo.
Staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael
‘ Lulu ’ akiangusha pozi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kina
makazi jirani na nyumba hiyo , baadhi ya
watu wanaojiita madalali wamekuwa
wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye
nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema
inauzwa na Lulu mwenyewe .
MCHEZO ULIVYO
“Baadhi ya madalali feki wamekuwa
wakiwaleta wateja wanaotaka kununua
nyumba maeneo haya. Wakifika wanasema
Lulu anaiuza , wakiwa wameshaiona wanatoa
fedha za usumbufu au za kuwapoza
wasipeleke watej wengine na kutoa namba
feki ya Lulu ili mteja ampigie.
“Wapo wateja walishanifuata na kusema
wanampigia Lulu hapatikani , lakini
waliponionesha namba yenyewe si ya Lulu .
“Siku moja mteja mmoja aliletwa na dalali
kuiona nyumba , akaipenda , akampa dalali
shilingi 300 ,000 za kumfanya asipeleke
wateja wengine , akampigia Lulu
hakupatikana. Alipokuja kwangu nikaiangalia
namba hiyo ilisajiliwa kwa jina la
Mwanahamis nani sijui ,” kilisema chanzo
hicho.
MAPAPARAZI WAJIFANYA WATEJA,
MADALALI WASHTUKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapaparazi
wetu walijifanya wateja wa kuinunua nyumba
hiyo na kwenda kukutana na watu wawili
waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na
Mambeze ‘ Mchopa ’ .
Baada ya mazungumzo, madalali hao walidai
kuwa , funguo za kuingia ndani ya nyumba
hiyo anazo mama Lulu ( Lucresia Karugila ) na
alisema angefika siku hiyo saa kumi jioni na
kuwataka mapaparazi kurudi muda huo .
Wakati mapaparazi wetu wanaondoka , dalali
mmoja alisema : “Nyie kama mmekuja
kututega mmeliwa wenyewe, hapa hakuna
mtoto wa kijijini. Wanaokuja hapa kutaka
nyumba wanajulikana , nyie mmetumwa. ”
LULU ALISHAFIKA , HAJUI KITU
Sosi mwingine alisema hivi karibuni alimuona
Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia
nyumba hiyo ambayo imesimama ujenzi
lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya
kuiuza !
“Mimi mara ya mwisho nilimuona Lulu eneo
hili na gari lake, naona alikuja kuangalia
nyumba inaendeleaje na usalama pia. Mambo
ya kuwa anaiuza hata siyajui ingawa kweli
hata mimi nimekuwa nikiwaona watu wakija, ”
alisema sosi huyo ambaye hakutaka jina lake
lichorwe gazetini .
Juzi , gazeti hili lilimsaka Lulu kwa njia ya
simu kwa ajili ya kumuuliza kuhusu suala hilo
ambapo, awali aling’ aka, akasema:
“Wewe ndiyo unaniambia kusema ukweli, sijui
chochote. Naomba mnipe habari kwa upana
ilivyo maana nyie waandishi mara nyingi
mnakuaga wa kwanza kujua habari kuliko
mhusika.”
Amani: Wewe Lulu sema ukweli tu , kama
unaiuza. Nilichokwambia ndicho.”
Lulu: Kweli mimi siiuzi nyumba yangu wala
sina wazo . Huyo aliyewapa habari awape
kwa undani ili nijue .”

0 comments:

Post a Comment