WEMA KIBOKO


WEMA Isaac Sepetu ‘ Beautiful Onyinye’
ameonesha ni kiboko katika sekta ya urembo
baada ya kuibuka kidedea kwenye shindano
bab’ kubwa la kumsaka staa wa kike Bongo
mwenye mvuto ‘ Ijumaa Sexiest Girl 2013 - 14’ .
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful
Onyinye’ akikabidhiwa tuzo ya ‘ Ijumaa
Sexiest Girl 2013 - 14’ na msanii Nikki wa
Pili .
Fainali za shindano hilo zilifanyika mwishoni
mwa wiki iliyopita ndani Ukumbi wa Dar Live
uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo
Wema alikuwa akichuana na warembo
wengine, Jokate Mwegelo , Jacqueline Wolper ,
Elizabeth Michael ‘ Lulu’ na Nelly Kamwel
‘ Dokyumetari’ kwanza
Kabla ya kumtangaza mshindi, maelfu ya
watu waliokuwa wamefurika ndani ya ukumbi
huo, walipata fursa ya kupata maelezo ya
kila mshiriki aliyeingia ‘ top 5’ sambamba na
picha zao kali za mnato kupitia screen
kubwa , hali iliyoamsha shauku ya kutaka
kumjua mshindi. hariri aelezea mchakato.
Wema Isaac Sepetu ‘ Beautiful Onyinye’
akisalimiana na mashabiki wake .
Baada ya mashabiki kuangalia ‘ dokyumentari’
hiyo , Mhariri wa Gazeti la Ijumaa ambalo
ndilo lililokuwa likiendesha shindano hilo,
Amran Kaima alitoa maelezo kuanzia
mwanzo wa shindano na njia zilizotumika
kupiga kura hadi kumpata mshindi .
“Shindano lilianza tangu mwezi wa tano,
mwaka jana, wasomaji wa Gazeti la Ijumaa
walipiga kura kupitia namba ya simu ya
gazeti, Mtandao wa www .
globalpublishers. info, mitandao ya kijamii na
barua pepe .
. ..Akiwapungia mashabiki mkono baada ya
kutangazwa mshindi.
“Mchuano ulikuwa mkali na hata warembo
walioingia tano bora ilikuwa vigumu kutabiri
mshindi kwani wote ni wakali, ” alisema
Kaima.Nikki wa Pili atangaza mshindi
Baada ya maelezo ya mhariri , msanii kutoka
Kundi la Weusi , Nickson Simon ‘ Nikki wa Pili’
aliyepewa dhamana ya kumtangaza mshindi
aliitwa stejini ili kumaliza mchezo .
Wema akiwa na tuzo yake .
Bila kupoteza muda , Nikki alifungua bahasha
iliyokuwa na jina la mshindi na Wema
alionekana kung’ ara hivyo kuibua
shamrashamra kuashiria kuwa , mrembo huyo
mwenye figa bomba na sura ya kuvutia
alistahili kuvaa viatu vya mshindi wa mwaka
2012/13 , Jacqueline Wolper .
Mbali na tuzo aliyopewa Wema , pia
aliahidiwa shilingi milioni moja ambazo
angepewa baada ya shindano hilo.
Baada ya Wema kutangazwa mshindi ,
burudani ya kufa mtu ilianza kuporomoshwa
kutoka kwa Kundi la Wanaume Family na
Weusi ambao walinogesha fainali hizo .

0 comments:

Post a Comment