Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch
anaripoti kwamba wakazi wa jiji la Eldoret
wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na pengine
kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara ya
kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki
barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret
kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni
maandalizi ya kumlaki nabii Daktari Awuor kwa
ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu
kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa
kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa
amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya
kijamii maoni yalikotolewa na Wakenya kuhusu hii
ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo
cha waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa
kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki
Radio ya kass fm inayotangaza kwa lugha ya
kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la
Eldoret Julius lamaon, amesema ‘watu wetu
waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na kuwa
jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria
mkutano huu’
WAUMINI WASAFISHA BARABARA KWA SABUNI
10:53 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment