UNATAKA KUMUOA JOHARI?SOMA HAPA! ....Part1

Julai 28 , 1983 mkoani Shinyanga , alizaliwa
mtoto wa kike ambaye sasa ni staa mkubwa
wa filamu za Kibongo. Ni maarufu kwa jina
la kistaa la Johari lakini majina yake kamili ni
Blandina Changula .
Kama kawaida yetu huwa tunatoa nafasi kwa
staa kusimulia alikopitia hadi akafikia
mafanikio aliyonayo ili kutoa chansi kwa
Blandina Changula "Johari " akiwa kwenye
pozi
wengine kujifunza au kutamani kuwa kama
yeye. Yaani kutoka ‘ ziro’ hadi ‘ hiro ’ . Leo
tunaye Johari kwenye spesho intavyu .
UNGANA NAYE.
Sifael: Johari ni nani?
Johari: Ni staa mkubwa wa Bongo Movies .
Sifael: Elimu yako ni ipi ?
Johari: Nimepata elimu yangu ya msingi
mkoani Shinyanga katika shule iitwayo
Bugoyi.
Nilihitimu mwaka 1996 . Baadaye nilipata
elimu yangu ya sekondari kwenye shule
inayoitwa Buluba kulekule Shinyanga kabla
ya
kuja kumalizia elimu yangu kwenye Shule ya
Greens ya Dar .
Nilipomaliza kidato cha nne nilisomea mambo
ya ‘ usekretari’ na baadaye nilisomea mambo
ya hoteli hapahapa Dar .
Sifael: Ulianza lini mambo ya kuigiza ?
Johari: Nilianza kujiingiza kwenye mambo ya
sanaa tangu nikiwa mdogo . Nilianza kuigiza
nikiwa shule ya msingi na kanisani .
Nilipenda kuigiza tangu nikiwa mdogo .
Sifael: Ulianza lini kuigiza rasmi ?
Johari: Nilianza kuigiza rasmi kupitia Kaole
Sanaa Group pale Kigogo , Dar . Nilienda kwa
mara ya kwanza kwenye kundi hilo
nikaomba fomu ya kujiunga na kuanza
kufanya mazoezi ya kuigiza .
Sifael: Unakumbuka ilikuchukua muda gani
wa mazoezi hadi ukaonekana runingani?
Johari: Ilinichukua kama mwaka mzima
nikifanya mazoezi na kundi hilo kabla ya
kupata nafasi ya kuigiza rasmi kwenye
michezo
ya runinga .
Sifael: Ulikuwa na akina nani?
Johari: Nyota yangu ilianza kung’ aa
nilipokuwa na Steven Kanumba ( kwa sasa
marehemu) na Vincent Kigosi ‘ Ray ’ ambao
walinishawishi kuachana na michezo ya
runingani na kuanza mchakato wa kufanya
filamu .
ITAENDELEA WIKI IJAYO

0 comments:

Post a Comment