Staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf
‘ Batuli’ na mwenyekiti wa Klabu ya Bongo
Movie , Steve Mengere ‘ Steve Nyerere ’
wameingia kwenye bifu zito baada ya
kutofautiana katika makubaliano ya kikazi.
Yobnesh Yusuf ‘Batuli ’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni
wawili hao waliingia kwenye mabishano
wakati Steve Nyerere alipokuwa akiandaa
filamu yake mpya iitwayo Get Out ambapo
alipaswa kumshirikisha Batuli.
Ilisemekana kwamba jamaa huyo alipompigia
simu, mwanadada huyo alichomoa baada ya
kuona makubaliano ya kifedha
hayazungumziwi .
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo
Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere ’
“Batuli alipohoji kuhusu malipo , Steve
hakuweka wazi ndipo mambo yalipoharibika ,
kikanuka kisha Batuli akamvaa kwa maneno
kiongozi huyo na kudai hana sifa za kuwa
kiongozi , ” kilisema chanzo chetu .
Ili kujiridhisha na madai hayo, mwanahabari
wetu alimwendea hewani Batuli ambapo
alipatikana na kukiri kuwa ametofautiana na
Steve chanzo kikiwa ni filamu hiyo .
“Aliponipigia simu nilimwambia sitaweza
kwenda kushuti kwa sababu hakuna
makubaliano yoyote tuliyofanya ikiwemo
gharama , usafiri , mavazi na vinginevyo ndipo
akamaindi na kuanza kulaumu na kisha
kukata simu, ” alisema Batuli.
Ishu haikuishia hapo , taarifa zinadai kuwa
baada ya Steve kutofurahishwa na majibu ya
Batuli, aliendelea kumtumia meseji za
kumlaumu ndipo Batuli alipochachamaa zaidi
kwa kujibu mashambulizi.
Staa wa sinema za Kibongo , Yobnesh Yusuf
‘Batuli ’
“Steve anapaswa akasomee utawala na
uongozi bora kwani hafai kuwa kiongozi ,
hana busara , kwa sababu kabla sijagombana
naye nilikuwa nikisikia maneno na majungu
ila baada ya ugomvi wangu na yeye
nimegundua hafai , ” alisema Batuli na
kuongeza : “Ananiambia mimi ni msanii
mchanga ilihali mimi kwenye kiwanda nipo
kwa miaka kumi na nne na mwaka 2, 000
wakati naanza yeye alikuwa anachekesha
watu ili apate kula kwanza nimemdharau
kwa sababu amekuwa akinichonganisha na
wasanii wa Bongo Movie eti mimi
nimewaambia wanajiuza .”
Baada ya Batuli kufunguka , gazeti hili
lilimgeukia Steve Nyerere na kumsomea
madai hayo ambapo alifunguka : “Sipendwi na
watu na sijui nini tatizo, nikiwa kama dairekta
nina uwezo wa kumchagua huyu nifanye naye
kazi na huyu kumuacha ,
yule ( Batuli) kama analeta chuki basi zitakuja
hivyo basi ni nyingi tu , ’’ alisema Nyerere na
kuongeza :
“Kwa heshima niliyoitengeneza kwa miaka 32
alafu nije nigombane na mwanamke, kwanza
nagombana naye nini? Nashukuru nimepata
ushauri , naendelea na kazi ya kutetea
maslahi ya Bongo Muvi kama ni filamu mimi
nilishachezesha msanii mwengine . ”
BATULI NA STEVE KIMENUKA
2:08 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment