TID, RECHO THT WADAIWA NI WAPENZI


MALOVEE ? Bosi wa Top Band , Khaleed
Mohamed ‘ TID ’ au ‘ Mzee Mnyama ’ na mtoto
mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania
( THT) , Winfrida Josephat ‘ Recho THT’ ,
wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa ni
wa kimapenzi , Ijumaa Wikienda limeinusa .
Mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji
Tanzania ( THT ) , Winfrida Josephat ‘ Recho
THT ’
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao
wamekuwa wakionekana pamoja sehemu
mbalimbali huku wakidaiwa kupiga ‘ mitungi’
kiasi cha kushindwa kuzificha hisia zao.
Bosi wa Top Band , Khaleed Mohamed ‘ TID’
au ‘ Mzee Mnyama ’ .
“Mbona ipo wazi , TID na Recho siku hizi
hawafichi kitu , tena wanapopiga mitungi
ndiyo kabisa , mfano mzuri ni juzikati
walikuwa pamoja mjini Dodoma , waliponda
raha kinomanoma, ” kilitiririka chanzo hicho.
Kama ilivyo ada , wanahabari wetu waliingia
mzigoni kwa kuanzia nyumbani kwa Recho ,
Kinondoni, Dar , wakamkosa lakini badala
yake, walipatikana mashosti zake wa karibu .
“Recho kwa sasa anatoka na Mnyama na
hapa tunavyoongea yupo Njombe ambapo
ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na
TID kuzagaa mtaani, halafu pia Recho siku
hizi anapombeka sana na tunahisi hata
‘ mambo meupe’ anatumia, ” alisema shosti
huyo.
Baada ya kushibishwa data hizo , waandishi
wetu walitinga ofisini kwake THT , Kinondoni
ambapo wanamuziki wenzake walisema staa
huyo ana muda mrefu hajafika kazini hapo
pasipo kutoa sababu za msingi.
Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho ,
akafunguka :
“Kweli nakunywa pombe lakini si kiivyo watu
wanavyonisema . TID ni mtu wangu kikazi
wala siyo kimapenzi . Watu wamekuwa
wakinishutumu kila ninapokuwa na
mwanaume wanasema ni bwana’ ngu kitu
ambacho si cha kweli kama wanavyonizushia
kuvuta bangi.
“THT siendi kwa sababu nimesafiri , hapa
ninapoongea nipo Njombe . Nimekuja kutulia
huku kutokana na maneno kuzidi na watu
kunipakazia uongo , ” alisema Recho .
Kwa upande wake TID , alipopigiwa simu,
alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho
kikazi na wala si vinginevyo.
“Dah.. .! Ebwana naomba uachane na hizo
habari za mapenzi, mimi ni mtu mzima nina
mengi ya maendeleo ambayo natakiwa
nifanye,” alisema TID .

0 comments:

Post a Comment