KAJALA : MWANANGU ANAJISIKIA VIBAYA MIMI KUITWA MALAYA


Staa wa Bongo Muvi , Kajala Msanja katika
pozi .
Maisha yanabadilika kwa spidi ya ajabu ndiyo
maana ukweli wa leo unaweza kuwa uongo
wa kesho !
Kwa kitambo kirefu mastaa wawili wa sinema
za Kibongo, Kajala Masanja na Wema Isaac
Sepetu walikuwa kama kumbikumbi . Marafiki
wa kufa na kuzikana . Sasa mambo
yamebadilika .
Walizoea kulala hadi kitanda kimoja. Walikula
na kunywa , walifanya kazi pamoja . Jioni
walikwenda kujirusha pamoja .
Kajala Masanja na Wema Sepetu .
KAMBI ZAIBUKA
Wiki kadhaa zilizopita upepo ulibadilika .
Kukawa na kambi mbili. Kila moja ikichafua
upande mwingine . Anayeumizwa zaidi ni
Kajala ambaye chanzo cha yote ni Sh . Milioni
13 alizolipiwa na Wema alipohukumiwa
kifungo cha miaka 7 jela au kulipa kiasi hicho
cha fedha kama faini.
Hoja ya kundi linalojiita Team Wema ni
kwamba Kajala anamuonesha Wema dharau
huku akitoka kimapenzi na yule kigogo wa
Wema aitwaye Clement au CK ili
kumchoresha mwanadada huyo ( wanamwita
Madam) . Ili kukata mzizi wa fitina ,
tunakuletea exclusive interview na Kajala
ambaye anafunguka mambo yote yaliyotokea .
UNGANA NAYE .. .
Wikienda: Kwa nini umegombana na Wema ?
Kajala : Sijagombana naye , labda yeye tu .
Wikienda: Inasemekana huzungumzi naye na
tayari ana mashosti wengine kama kina Aunt
Ezekiel na Snura Mushi . Je , ni kweli ?
Kajala : Nilichati na Wema kama siku tano
hivi zilizopita. Kuhusu marafiki, Wema ana
marafiki wengine wengi siyo mimi tu . Hata
wakati nikiwa naye alikuwa nao .
Wikienda: Umesema uliwasiliana na Wema
kupitia mtandao tena kama siku tano hivi
zilizopita. Kwa watu marafiki wa kufa na
kuzikana huoni kama ni tatizo ?
Kajala : Sielewi chochote !
Wikienda: Wewe na Wema mnagombea nini
hasa?
Kajala : Mimi nashangaa ghafla tu kundi la
watu linanitukana mitandaoni. Hata Wema
mwenyewe hawajui . Ishu ya milioni 13 ndiyo
imekuwa habari ya mjini.
Natukanwa sana . Mwanangu anashindwa
kusoma, anajifungia ndani na kulia siku
nzima kwa kusikia mama yake akiitwa
malaya ( maskini analia ) .
Unajua mwanangu amekua, anaambiwa na
kuona ninavyotukanwa hivyo lazima ajisikie
vibaya . Mwanangu anateseka, anafanya
vibaya darasani ( yupo darasa la saba) .
ANATAKA KURUDISHA MIL . 13?
Wikienda: Kuna taarifa kuwa unataka
kuzirejesha hizo Sh . milioni 13. Inasemekana
upo tayari kuuza gari lako jipya ( Toyota
Bravis ) . Kajala : Nitazirejesha vipi wakati
alinilipia hakunikopesha ? Sijui kama
inawezekana. Sijauza wala sina mpango wa
kuuza gari ili nikamlipe hizo Sh . milioni 13 .
TATIZO LILIANZAJE ?
Wikienda: Tatizo lilianzaje?
Kajala : Nakumbuka maneno yalianza baada
ya kwenda kufanya shoo Arusha. Tuliporudi
mwenzangu akaanza kubadilika . Baada ya
Arusha tulikutana tena saluni maeneo ya
Kinondoni ( Dar ) .
Nilifika pale na baiskeli, nilitokea location .
Nilikuwa na majasho sana si unajua
kuendesha baiskeli?
Kumbe yeye ( Wema ) alikuwa ghorofani
kwenye ile saluni .
Mimi nilikaa ili nipigwe na upepo au kiyoyozi
ili nikae sawa . Aliposhuka akaniona , alitaka
kunikumbatia. Nikamwambia nooo ... nina
jasho, akamaindi ileile na ku -shout ( kelele )
eti mimi nimekataa kumkumbatia .
KAMCHUKUA CLEMENT ?
Wikienda: Inasemekana wewe umemchukulia
aliyekuwa bwana’ ke Clement aliyeachana
naye , wewe ukaona umchoreshe hivyo
akamaindi, hilo likoje?
Kajala : Katika maisha yangu niliwahi kuonana
na Clement mara moja tu . Sina hata namba
yake ya simu , sasa sijui nimemchukuliaje !
USAGAJI
Wikienda: Inadaiwa wakati mkiwa na urafiki ,
mlikuwa mnashiriki mapenzi ya jinsi moja
( usagaji) . Je , ni kweli ?
Kajala : Ni kweli nikuwa nalala naye kitanda
kimoja, sasa hapo kwenye usagaji nani
‘ mwanaume ’ na nani mwanamke ?
Wikienda: Inasemekana wewe ndiye ulikuwa
‘ mwanaume ’!
Kajala : Huuh . .. hakuna kitu kama hicho.
ANAMCHUKIA DIAMOND?
Wikienda: Madai mengine yanasema
umekorofishana na Wema kwa sababu
karudiana na Nasibu Abdul ‘ Diamond
Platnumz’ na mara nyingi wanakuwa wote
chumbani hivyo unakosa nafasi ya kujiachia
naye . Je , ni kweli unamchukia Diamond ?
Kajala : Kwa nini nimchukie Diamond ? Sina
shida naye . Huwezi kumchukia binadamu
mwenzako hata kama kuna sababu .
Wikienda: Je , upo tayari kupatanishwa na
Wema ?
Kajala : Nipo tayari . Ninyi mkimpata na mimi
nikiwa na nafasi nitakuja Global nipatane
naye maana haya maneno na mimi
yananiumiza. Roho inaniuma jamani hata
mimi nina moyo wa nyama siyo chuma.

0 comments:

Post a Comment