HENRY KILEWO ATUPIA MTANDAONI CHAT YA WHATS APP YA RIDHIWANI NA JERRY SLAA WAKIMPONDA LOWASSA


Kwenye Ukarasa wa Facebook wa Henry Kilewo
leo asubuhi nimekutana na hili:
"Muoneni huyu anawaza kuwa Rais baada ya
kupewa ubunge.... never ever... RZ1
AMSHAMBULIA LOWASSA
RZ1 Jakaya Mrisho Kikwete, amemshambulia
Edward Lowassa na kumuita mlevi na kamwe
hataweza kuwa rais wa Tanzania baada ya baba
yake, Jakaya Kikwete. Katika mazungumzo yake
kwa njia ya Whatsapp kati yake na Jerry Slaa,
meya wa Manispaa ya Ilala, Ridhiwani anarejea
kauli yake ya miaka mingi kwamba, "Lowassa
akiingia Ikulu, mimi nitahama nchi."Ukifuatilia
kwa makini maelezo haya, utaweza kubaini
mapema kuwa Lowassa anapigwa vita na
Kikwete mwenyewe; Ridhiwani ni zumari la
Kikwete katika mapambano kati ya Lowassa na
yeye.RZ1 anafika mbali zaidi kwa kusema,
mgogoro kati ya Zitto Kabwe na chama chake,
umesababisha na Mwigulu kupandikiza watu
wao ndani ya chama hicho. Kutokana na
umuhimu wa hiki ambacho amekieleza, nimeona
ni vema niweke hapa MF ili watu wajadili." Henry
Kilewo

0 comments:

Post a Comment