Drake na Rihanna wanaendelea kushibana na
penzi lao linachanua huku wakiripotiwa kuwa na
mpango wa kuishi pamoja.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, chanzo
kimoja kimeeleza kuwa Drake amemnunulia
Rihanna zawadi ya pete ya almasi yenye rangi
ya njano yenye thamani ya $42,000 (sawa na
68,712,000/-).
Hata hivyo imeelezwa kuwa pete hiyo sio ya
uchumba.
“Rihanna aliikubali zawadi hiyo kama ishara ya
mapenzi ya Drake. Sasa hivi (Drake) anabadili
hata ratiba zake ili atumie muda mwingi
ipasavyo kuwa na Rihanna.” Kilieleza chanzo
hicho.
Drake na Rihanna wanaonekana kuwa karibu
zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda, na hata
Jumapili katika MTV Movie Awards walionekana
wakiwa wameshikana mikono muda mfupi baada
ya Drake kuperform.
DRAKE AMNUNULIA RIHANNA ZAWADI YA BEI MBAYA
1:12 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment