Well leo tumeamua ikuletee list ya watu
10 ambao now days wamekuwa
maarufu kupitilizalakini umaarufu wao
wote umetokana na mtu fulani
inamaana bila fulani wasingekuwa
maarufu na kuzungumzwa katika jamii
tuliyopo. tuanze countdown yetu kwa
kuanzia namba 1 hadi namba 10.
1. Agnes Masogange
Huyu alijipatia bahati ya kufahamika
kwa kasi baada ya msanii belle 9
kumtumia kwenye nyimbo yake ya
masogange ambayo Agnes alicheza
kama Masogange, hadi Leo
anafahamika kwa jina la masogange, ni
kati ya watu wanaozungumzwa sana
mitandaoni. Kesi yake ya madawa ya
kulevya ilimuweka kwenye ulimwengu
wa mastaa.
2. Romy Jones
Huyu jamaa ni ndugu wa Diamond.
Amefahamika sana baada ya kuwa
karibu na mwanamuziki Huyo,
japokuwa ana maringo na nyodo kuzidi
Diamond. Na yeye huyu sio
mwanamuziki wala mcheza filamu.
3.Penny
Huyu bidada ni mtangazaji wa Dtv.
Alikuwa hafahamiki apo awali, Jina lake
lilivuma sana na kujikuta akiingia
kwenye ulimwengu wa mastaa baada ya
kujihusisha kimapenzi na msanii
Diamond, ni miongoni mwa watu
wanaofuatiliwa sana na kuzungumzwa.
4.Mange kimambi
Huyu alipata umaarufu kupitia mastaa
kadhaa wa Tasnia mbali mbali apa
bongo, alianza kuzinguana kwenye
blogs na msanii wa maigizo Sintah, Ray
( kuhusu kifo cha Kanumba), Shigongo
na wengine kadhaa, wengi walitaka
kumjua ni mtu wa aina gani baada ya
kuanzisha bifu na mastaa wa bongo,
hatimaye akajikuta akiogelea umaarufu.
5.Chaga Barbie
Huyu alijipatia umaarufu baada ya
kujihusisha kimapenzi na msanii wa
Kenya Prezzo, jina lake lilivuma zaidi
pale walipozinguana na Prezoo hadi
kufikia hatua ya kutoleana maneno
mbofu mbofu mitandaoni. Ni kati ya
watu wanaofuatiliwa sana mitandaoni.
6.Petit man wakuache
Huyu jamaa amefahamika kupitia
Wema Sepetu, jina lake limevuma na
kutajwa tajwa sana baada ya kuwa
karibu na madame. Sio muigizaji wala
mwanamuziki.
7.Najma
Huyu ni ex wa Mr blue, nae alianza
kufahamika baada ya kujiingiza kwenye
mahusiano na msanii huyo. Scandal
yake ya kutoka na Diamond
ilimuongezea credit kwa kiasi flan na
kumfanya aongelew sana mitandaon,
alishawah kujarib mziki pia na filamu.
8.Clement
huyu alifahamika baada ya kujiingiza
kwenye mahusiano na super star Wema
Sepetu, ni kati ya watu
wanaozungumzwa sana mitandaoni
hadi kesho, japokuwa sura yake
haifahamiki kihivyo, bado watu
wanapenda kujua kuhusu yeye na
maisha yake.
9.Ostadh Juma
Watu mjini wanatafuta umaarufu kwa
kasi, baada ya kuzipata pesa kwa
wingi , aliamua Ku manage wasanii
kama PNC, dogo Janja na wengine
japokuwa hana management skills
nzuri. Kumrudisha dogo Janja dar es
salaam na kumweka kwenye kundi lake
la watanashati entertainment pamoja
na kumpiga picha PNC alipokuwa
akijaribu kumuomba msamaha
kumemfanya aongelewe zaidi na
kufuatiliwa maisha yake mbaya zaidi
hadi ya wazazi wake kitu ambacho
kimem cost kwa kiasi Fulani.
10. Kajala Masanja
Kwenye mtandao wa instagram ana
followers karibia elfu thelathini na kitu,
wote wametokana na promo ya maana
kwa shoga yake Wema Sepetu, kutolewa
rumande na Wema Sepetu
kumemuongezea umaarufu zaidi na
kuwa miongoni mwa watu
wanaozungumzwa sana, jina la kajala
limekaa sana mdomoni mwa Wema
Sepetu, hivyo kumfanya apate
mashabiki wengi zaidi kupitia Wema.
Ni mcheza filamu za kibongo.
MASUPER STAR WA BONGO WALIOTOKEA NA KUSAFIRIA NYOTA ZA WENGINE
4:32 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment