SHILOLE:NILIPONASA SASA SIPINDUI

STAA wa filamu na mduara Bongo, Zuwena
Mohamed ‘ Shishi Baby ’ amefunguka kuwa
amenasa vilivyo katika penzi la msanii
mwenzake, Nuhu Mziwanda hatarajii
kuachika .
S taa wa filamu na mduara Bongo, Zuwena
Mohamed ‘Shishi Baby ’ akiwa kwenye pozi
la kimahaba na mpenzi wake aliyefahamika
kwa jina la Nuhu Mziwanda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Shishi
alisema yupo tayari kuolewa na Mziwanda
kwani anampenda na ndiyo ubavu wake
kutokana na vile ambavyo amekuwa
akimwonesha mapenzi ya kweli tofauti na
wapenzi wake wote waliopita .
‘Shishi Baby ’ akiwa kwenye pozi na Nuhu
Mziwanda.
“Huyu ndiye shemeji yenu , ndiye mume
wangu mtarajiwa , ninampenda na yeye
ananipenda kwa hiyo Mungu akijalia soon
tutakamilisha taratibu za ndoa, ’’ alisema
Shishi Baby .

0 comments:

Post a Comment