RATIBA YA MAZISHI YA MZEE GURUMO NA SIKU ATAKAYOZIKWA


Taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo na
mtoto wa kwanza wa Marehemu Mzee
Gurumo Ndg Abdallah Gurumo
amesema kuwa leo saa 10 jioni
kutakuwa na kisomo hapa nyumbani
kwa Marehemu eneo la Tabata Kisukulu
ambapo Watanzania wote
wanakaribishwa.
Baada ya kisomo saa 3 ya asubuhi
kesho April 15 mwili wa Marehemu
utaletwa nyumbani kwa ajili ya swala
kisha saa 4 asubuhi safari ya kuelekea
kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe
Mkoa wa Pwani itaanza kwa ajili ya
maziko ya Mzee Gurumo.
Kwa mtu usiyepafamu nyumbani kwa
Mzee Gurumo ukiwa unatokea Ubungo
kabla ya Mwananchi kuna kituo
kinaitwa Garage shukia hapo kisha
ulizia mtu yoyote atakuelekeza pia kwa
wewe unaetokea Tabata, Buguruni au
Tazara shukia hapo Garage kituo baada
ya Mwananchi.

0 comments:

Post a Comment