SIKILIZA/SOMA HAPA CHANZO CHA KIFO CHA MZEE GURUMO NA MAZISHI YAKE KUFANYIKA LEO


Watoto wa marehemu wakiwa katika majonzi na
huzuni baada ya kumpoteza baba yao ambaye
amafariki dunia tarehe 13 april katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili baada ya kusumbuliwa na
matatizo ya moyo kwa kipindi kirefu.
Pia mdogo wa marehemu Ramadhani Mwishehe
na Mtoto Mwalim Muhidin Gurumo
walizungumza na sammisago,com wakielezea juu
ya kifo cha Muhidin Gurumo maarufu kama Mzee
Gurumo na mazishi yatakapofanyika Kisarawe
Masaki
“Baba yetu aliugua kwa muda mrefu sana
anaugua anapata nafuu anaugua anapata nafuu
siku ya mwisho jana saa kumi na moja alfajiri
alizidiwa pumzi ilikuwa zimembana tukampeleka
Hospitali Muhimbili pale, leo hii saa nane
mchana ndiyo anaaga dunia na prosesi za
mazishi zitakuwa kesho saa tano asubuhi na
atazikwa Masaki uzaramuni” Mtoto wa
Marehemu Mwalim Mwidin Ngurumo.
Mdogo na Mtoto wa Marehemu walizungumza
haya:

0 comments:

Post a Comment