ROSE MUHNDO YAMEMKUTA

MY GOD ! Mwanamuziki wa Injili daraja la
kwanza nchini , Rose Muhando anaishi roho
mkononi kufuatia madai kwamba kuna watu
wanaomsaka wakisemekana wametumwa
kuichukua roho yake, Ijumaa Wikienda lina
kisa kizima .
Mwanamuziki wa Injili daraja la kwanza
nchini , Rose Muhando.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Rose anaishi
kwa machale jijini Dar akikimbia Dodoma
baada ya taarifa kwamba mtu mmoja
aliyetajwa kwa jina moja la Nasani na
wenzake wanataka kumdhuru kama si
kumtoa roho kabisa .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion , Alex Msama aliyepata ajali
inayohusishwa na watu wenye nia ya kutaka
kumteka Rose Mhando.
“Hao watu si wazuri ! Mara kwa mara
wamekuwa wakiandaa mikakati ya kumfanyia
kitu kibaya Rose .
“Mfano mzuri ni Aprili 3 na 4, mwaka huu ,
watu hao waliweka mtego wa kumteka Rose
kwenye hoteli moja jijini Dar es Salaam,
wakashindwa kutokana na mazingira, ”
kilisema chanzo hicho.
Alex Msama akiwa amelazwa mara baada ya
kupata ajali.
TUKIO BICHI
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa
baada ya watu hao kushindwa kufanikisha
zoezi hilo siku mbili hizo , Aprili 6 ( mwaka
huu) walijipanga tena kumvamia Rose katika
tamasha la Injili alilolifanya kwenye Kanisa la
KKT- Usharika wa Magomeni -Mapipa jijini
Dar .
“Tulisikia kuwa kuna watu wametumwa ,
wakafikia katika gesti moja iliyopo Magomeni
Mwembechai ( jina lipo) lakini walishindwa
kutekeleza azma yao hiyo kwani tayari timu
ya Rose ilishapewa taarifa hivyo akajiandaa .
Pia waliogopa zaidi baada ya kumwona mtu
mmoja amekaa meza kuu akiwa amevalia
mavazi ya kijeshi, tena mwenye cheo cha juu
maana alikuwa na nyota begani, ” kilisema
chanzo.
Kikaongeza: “Siku hiyo timu ya Rose
haikuripoti polisi juu ya tukio hilo kwani
tayari walishawahi kutoa taarifa kwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu baada
ya Rose kutishiwa maisha na huyo Nasani. ”
CHAMA CHA WAIMBA INJILI CHAPEWA
TAARIFA
Taarifa zaidi zilidai kuwa uwepo wa taarifa
za Rose kutaka kutekwa Magomeni zilimfikia
Katibu wa Chama cha Waimba Injili
Tanzania , Stella Joel ambaye naye
alipoongea na gazeti hili alikiri kuzipata hizo .
Stella : “Tulisikia mapema kwamba kuna watu
wametumwa kuja kumteka Rose . Tamasha
siku hiyo lilianza saa nane mchana lakini sisi
tulituma ‘ mashushushu’ wetu saa tatu
asubuhi kukagua mazingira. Kweli , wakati
tamasha limeanza kuna muda waliingia watu
watatu, wakaangazaangaza huku na kule
kisha wakatoka.
“Tunamshukuru Mungu hakuna jambo baya
lililotokea ingawa tulikaa kwa tahadhari
kubwa , ” alisema Stella .
Paparazi: Tunasikia walikuta mwanajeshi wa
cheo cha juu amekaa meza kuu wakaogopa,
ni kweli ?
Stella : Hapana , yule si mwanajeshi . Ni
muimba Injili anaitwa Mwanamapinduzi .
Huwa anapenda kuvaa kama mwanajeshi .
AJALI YA MSAMA YAHUSISWA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga madai zaidi
kwamba hata ajali aliyoipata Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotion , Alex Msama
mkoani Dodoma , Ijumaa iliyopita, ilipangwa
na huyo Nasani. Habari zinadai kwamba
Nasani hakupenda Rose ashiriki katika
Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na
Kampuni ya Msama kwa sababu yeye ana
bifu naye .
Ilidaiwa kuwa , Machi 8 , mwaka huu Nasani
na Msama walifanya kikao cha kujadili Rose
atoke kwenye Tamasha la Pasaka , lakini
muandaaji huyo alikataa .
ROSE NA NASANI KUNA NINI?
Ikaendelea kudaiwa kuwa miaka kadhaa
iliyopita, Rose na Nasani waliwahi kufanya
biashara ya pamoja ( haikutajwa) lakini
waliposhindwana hawakuachana vizuri na
ndiyo maana jamaa huyo amekuwa mstari
wa mbele kuhakikisha anamdidimiza
mwimbaji huyo mahiri Bongo.
NASANI ANASEMAJE?
Juzi paparazi wetu alimtafuta Nasani kwa
njia ya simu, alipopatikana alisema :
“Hilo tukio la Rose kutaka kutekwa ndiyo
nalisikia leo . Sasa mimi nimteke Rose ili
iweje ? Siwezi kufanya hivyo na wala sihusiki
kabisaaa.
“Kuhusu ajali , siku moja kabla ya tukio mimi
nilikuwa na Msama , akaniambia anakwenda
Dodoma , mimi nikamwambia nitaondoka saa
5: 20 na basi asubuhi yake , yeye alitangulia
kwa gari binafsi . Nilipofika Chalinze , mke
wake akanipigia simu na kuniambia mumewe
amepata ajali , sasa hapo mimi nahusikaje ?
“Nahisi kuna watu wananizushia mambo ili
kunichafulia jina langu maana kuna meseji za
vitisho nimetumiwa .
KUHUSU ROSE
Kwa mujibu wa Stella , Rose alisema yeye
anamuamini Mungu kuwa hakuna
atakayeweza kumuangusha lakini pia
anajivunia uwepo wa taarifa zake kwa IGP .
Kuhusu tukio la Magomeni , Rose alisema
hajui chochote labda kwa vile alikuwa
akipafomu jukwaani .
Hata hivyo , juzi paparazi wetu alimpigia simu
Rose mara tatu bila kupokelewa. Mara ya nne
ilipokelewa , lakini mawasiliano yakawa
mabovu .

0 comments:

Post a Comment