Peter: Forever P-Square – Paul: P-Square stronger than Ever!!!


Mapacha wa P-Square wameongea na
inaonekana amani imerudi Squareville. Peter na
Paul wametumia mtandao wa Twitter kueleza
msimamo wa kundi lao na kwamba halijavunjika
na haliwezi kuvunjika kamwe.
Peter na mkewe Lola
Paul anayetumia @rudeboypsquare kwenye
Twitter ameandika: PSQUARE! Stronger than
Ever!!! na Peter anayetumia jina @PeterPsquare
akiandika: FOREVER PSQUARE!
Awali, Peter alidaiwa kugoma kuondoa kinyongo
chake kwa kaka zake akiwemo Paul licha ya
kuombwa sana marafiki zake.
Pacha huyo alisema kama familia inataka kuwa
na amani ni lazima imkubali na kumheshimu mke
wake Lola. “Peter amechoka kutokana na kutumia
miaka mingi kuiomba familia yake imkubali
mwanamke aliyeamua kumuoa. Anataka Lola
akubalike kwenye familia kama Anita (mke wa
Paul) alivyokubalika bila kuzingatia utofauti wa
umri wao,” chanzo kilicho karibu na familia hiyo
kililiambia gazeti Vanguard.
Paul na mkewe Anita
Vyanzo vilisema kuwa ugomvi wao ulikuwa
mkubwa zaidi baada ya kubainika kuwa Peter
amemnunulia nyumba Lola nchini Marekani.
Vanguard limedai kuwa kwa sasa Paul na Peter
wameanza kuongea tena japo Paul hajaonesha
kukubali ombi la pacha wake kwakuwa hata
mama yao kabla hajafa alikuwa hajakubali
uhusiano wa Peter na Lola.
Katika hatua nyingine Kaka yao Jude Okoye
ambaye anadaiwa kuwa na mchango mkubwa wa
ugomvi wa Peter na Paul, alitweet kueleza kuwa
kwake familia ni kitu cha kwanza na kwamba P-
Square itadumu.

0 comments:

Post a Comment