Sababu za D.Knob kufunga ndoa ya kimyakimya.


Hit maker wa single mpya ya Nishike mkono D
knob leo ame-amplify sababu za kuamua
kufunga ndoa ya kimya kimya mwaka 2009
huku idadi ya watu waliohudhuria pamoja na
maharusi wenyewe ikiwa sio zaidi ya 10
kuanzia kanisani mpaka walikoelekea baada ya
kutoka kanisani.
Ameongea na millardayo.com na kusema
‘nilitaka kuifanya na mwenzangu nikamwambia
tumekua wapenzi lakini sasa yahitaji tuwe
ndani ya ndoa akasema twenzetu
tukaongozana mpaka kanisani padri akasema
hamuwezi kuoana nyie mnajua hata ndoa ni
nini?kuna hatua’
‘Siyo kitu ambacho tulitaka kufanya kama
watu wengi wanavyofanya ile kukaa
kuchangishana kwa sababu mimi rafiki zangu
wa karibu wote walikua block nisingetaka
kufunga ndoa halafu mwisho wa siku tuanze
kununiana kuwa huyu hajachanga yule
kachanga chapili nilitaka kufanya ili niendelee
na maisha yangu kama mtu unapoamua
kufanya birthday’
‘Wazazi walipata taarifa mwishoni kwa sababu
hata mzee katika risala yake maana tulikaa
kwenye meza moja baada ya ndoa mzee
akasema mimi sijui nakupa zawadi gani maana
umeniambia jana tu,kitu tulichofanikiwa ni
gauni la mke wangu maana ni gauni la
gharama nashukuru Mungu lilitupa stress
mwanzo lakini liliwahi’.

0 comments:

Post a Comment