ODAMA AJIFUNGUA KIDUME

HABARI njema ! Staa wa sinema za Kibongo,
Jenifer Kyaka ‘ Odama ’ amejifungua kidume
huku akikataa kumtaja baba wa mtoto huyo .
Staa wa sinema za Kibongo, Jenifer Kyaka
‘Odama’ .
anayedaiwa kwamba ni mheshimiwa
serikalini .
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Odama
alijifungua kwa operesheni hivi karibuni
kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar baada
ya kuwa kimya kwa miezi kadhaa kutokana
na likizo ya uzazi ambayo ilimfanya asimame
kuigiza filamu kwa muda .
Jenifer Kyaka ‘Odama’ akiwa kwenye pozi.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo , gazeti
lilimtafuta kwa njia ya simu ambapo alikiri
kujifungua mtoto wa kiume na kwamba
anamshukuru Mungu kwani yeye na
mwanaye wanaendelea vizuri.
“Namshukuru sana Mungu na mimi sasa
naitwa mama. Hayo mengine ya baba mtoto
tuyaache muda ukifika mtamuona, ” alisema
Odama .

0 comments:

Post a Comment