MASOGANGE, WAKISEMA UNAJIUZA UTAKATAA ?


AGNES Jerald , binti anayetumika sana
kunengua na pozi katika video za nyimbo za
wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi
kipya , amejipatia umaarufu mkubwa sana
baada ya kufanya kazi na mkali wa
Morogoro, Belle 9 katika kibao chake cha
Masogange .
Limegeuka kuwa jina lake na mwenyewe
analitumia kikamilifu katika harakati za
kimjini . Lakini aligeuka kuwa kipusa zaidi
baada ya kukamatwa katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini
Johannesburg mwaka jana, akiwa na shehena
kubwa ambayo Tanzania ilijulikana kama
madawa ya kulevya, lakini Afrika Kusini
wakasema ni malighafi inayoweza kutumika
kutengeneza mihadarati.
Masogange ni msichana ambaye Mwenyezi
Mungu amemjaalia uzuri wa asili wa Kiafrika .
Ana sura nzuri ambayo bado hajaanza
kuikoboa kwa mikorogo na mwili unaoendana
na umbo lake maridhawa.
Sifa moja kubwa ya uzuri wa msichana huyu ,
ni maumbile yake ya nyuma , amejazia kiasi
ambacho ni wanaume wachache , tena walio
waadilifu kwelikweli , wanaoweza kupishana
naye na wasigeuke nyuma kuhakikisha
walichokiona!
Baada ya kuachiwa kutoka mahabusu nchini
Afrika Kusini ambako alishindwa kesi ya
kukutwa na shehena ile ya madawa ya
kulevya, Masogange alijikuta akiwa gumzo
kubwa jijini Dar es Salaam, kiasi kwamba
pamoja na kuachiliwa, bado ilimchukua muda
mrefu kurudi nyumbani .
Akiwa huko kwa Madiba , binti huyu alikuwa
akiweka picha zake kila mara katika
mitandao ya kijamii inayopatikana katika
Internet , hasa Instagram. Ni utamaduni mpya
kwa wasichana wa Kibongo siku hizi , wengi
wanapenda kutupia picha zao humo na watu
ambao huwaona , huwasifia kama
wamependeza au huwaponda kama
wamechukiza.
Lakini katika hali isiyotarajiwa kabisa , wiki
kadhaa zilizopita, Masogange aliweka picha
yake huko, ikionyesha sehemu kubwa ya
mwili wake, ikiwa imepakwa hina.
Aliipaka kwa staili ambayo mtu akiitazama
haraka haraka anaweza kudhani ni Tattoo, ile
michoro inayochorwa kwa sindano mwilini
ambayo hapo awali tulianza kuiona kwa
wasanii wa Kimarekani .
Lakini kitu kibaya katika picha hiyo ni
kwamba Masogange amepiga picha mguu
wake akiwa amepaka hina hiyo hadi juu
kabisa pajani .
Baadaye akapiga picha nyingine akiwa
amevaa kimini , lakini kikionyesha sehemu ya
paja hilo lililopakwa urembo huo ambao pia
hutumiwa na wanawake wa Kiislamu wakati
wa ndoa !
Ni picha ambayo mwanaume yeyote mkware
akiiona, anavuta hisia za mahitaji ya
kimapenzi . Na nieleweke, siyo Masogange tu
anayetupia picha za aina hii , wasichana
wengi hufanya hivi na baadhi yao, baada ya
kuziweka , huweka pia na namba zao za simu,
ukiwa na shida nao uwatafute !
Sitaki kuamini moja kwa moja kwamba
msichana huyu ambaye amepata umaarufu
bila ya kutarajiwa anajiuza, lakini ni vigumu
sana kwa picha zile kuacha kusadiki jambo
hili kama mtu mmoja atajitokeza na kutoa
madai kama hayo.
Inakuaje mtoto wa kike, mwenye jina, tena na
uzuri wako bomba kabisa wa asili , unapiga
picha za namna ile na kuziweka hadharani ?
Nafikiri siyo sawa , zipo picha zinazopaswa
kuendelea kubakia chumbani .
Kwa jinsi mambo yanavyotokea, unapata
kabisa hisia kwamba kumbe dada zetu
wanatafuta umaarufu kwa nguvu kwa
malengo binafsi, yasiyo ya kimaadili na yenye
kuchefua.
Wakishapata majina na bahati nzuri kuanza
kufuatiliwa na vyombo vya habari,
vikitanguliwa na magazeti , wanaanza
makeke!
Kwa kutambua kwamba sura zao
zinafahamika , badala ya kujistahi, ndiyo
kwanza utashangaa kuona wanavaa mavazi
yenye utata , kumbe tunaanza kuelewa kuwa
wanafanya hivi ili kujitangaza , kama
wanavyosema mabingwa wa uchumi,
biashara matangazo .
Ndiyo maana nimejikuta tu nikijiuliza, hivi
Agnes akiambiwa kuwa anajiuza kupitia
mitandao ya kijamii , atakataa ?

0 comments:

Post a Comment